EDWARD Lowassa: CCM Isijidanganye

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ameitaka CCM iache kujidanganya kuwa haiwezi kuondoka madarakani akiitaka iangalie alama za nyakati hasa mabadiliko ya uongozi yanayotokea kwingineko duniani.

Hata hivyo, Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amesema unahitajika muungano wa dhati wa vyama na uliopangiliwa vizuri katika juhudi za kuiondoa CCM madarakani.

Lowassa alisema hayo alipoombwa na mwandishi wa habari hizi kutoa tathmini ya maisha yake ya kisiasa mwaka mmoja na nusu tangu alipojiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA ambako aliteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho akiwakilisha muungano wa vyama vinne – CHADEMA, CUF, NCCR - Mageuzi na NLD – Iliopewa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtazamo wa kuangalia chama auleti maana, Bali walio wenye kujielewa wanangalia kiongozi bora si chama, kama ni chama hata yeye Lowasa alikuwa mwana ccm, na alishasemaga hawezi hama ccm, alihama tu pale, alipoona ametolewa mbali kwenye mchakato wa Urais, na khali yeye anautaka huo uraisi kwa khali na Mali, tumesha wachoak Hawa viongozi waliopita za awamu Karibia zote za huko nyuma, hamna waliyoyafanya zaidi ya ufisadi, tu na kuishi maisha ya kifahari, na kuwaacha watanzania wengi wakitabika na hata kukosa huduma muhimu kutokana na korruption zao

    ReplyDelete
  2. Kwani veepe, mbona kama swali na jibu vinatofautiana?? Au network bado 'chenga-chenga' hahahaha!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad