Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, ametaka vijana wa chama hicho kukabiliana na ukandamizaji wa demokrasia aliodai unafanywa na watawala.
Alisema hayo juzi alipokutana na vijana wa chama hicho ambao ni wanavyuo (CHASO) wa vyuo vikuu mkoani hapa.
Lowassa ambaye yuko Tabora kwa ziara ya kuimarisha chama, aliwataka vijana hao kuwa na ujasiri wa kukabiliana na ukandamizaji wa demokrasia kwani vijana duniani ndio chachu ya mabadiliko.
“Nimekuja Tabora kuwashukuru kwa kura nyingi mlizonipigia na hamasa kubwa mliyoionesha kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Katika uchaguzi ule tulishinda, lakini ushindi mkubwa zaidi ni tulipofanikiwa kuvumilia na kuweka maslahi ya watoto, wazee na mama zetu mbele," alisema na kuongeza:
"Amani ni tunu muhimu sana kwa mustakabali wa Taifa kuliko kitu kingine chochote. Msikate tamaa, tumejipanga vema kwa uchaguzi ujao wa mwaka 2020 na hatutadhulumiwa tena haki yetu, kama ilivyokuwa mwaka jana,” alisema Lowassa.
Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani, alisema Jambo Kuu na la msingi ambalo wana Chadema wanatakiwa kuwa nalo sasa katika chama ni umoja na mshikamano kati yao.
"Umuhimu wa umoja na mshikamano ndani ya chama chetu ni mkubwa sana, hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inajaribu kwa kila namna kukandamiza Upinzani na demokrasia na jambo hili si geni, ukirudi nyuma katika historia ya vyama vya siasa nchini, hata kabla ya Uhuru, unaweza kuona umoja ulivyoisadia TANU dhidi ya chokochoko za chama alichoanzisha mkoloni wakati ule - United Tanganyika Party (UTP) kukabiliana na kuidhoofisha TANU na kumzuia Mwafrika kupata Uhuru na kujitawala," alisema.
Aliwaambia vijana kwamba changamoto kama hizo ni za kawaida kwa vyama vingi vya upinzani hasa Afrika, ambavyo vinaungwa mkono na wananchi wengi wakiamini ni vya ukombozi.
Lakini pia alisema katika kujenga umoja na mshikamano huo ndani ya chama, ni lazima nguvu kubwa ipelekwe kwenye matawi waliko wananchi.
"Katika chama chochote cha siasa watu wengi hawako ngazi za juu, bali mashinani. Ni lazima nguvu yetu kubwa ielekezwe huko kwa sasa, ili kuhakikisha chama kinakuwa na misingi madhubuti ambayo inaweza kutumika kukisaidia nyakati za uchaguzi," alisema.
Aidha, Lowassa ambaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana alipata asilimia 38 ya kura, alihoji umuhimu wa Serikali kununua ndege zaidi, kuliko kupeleka huduma muhimu vijijini.
"Tumesikia nia njema yao ya kuagiza ndege nyingine zaidi miaka miwili ijayo, lakini tunajiuliza, je isingekuwa busara kutumia fedha hizo kupeleka maji safi na salama mijini na vijijini?" Alihoji.
LOWASSA Ahoji Uamuzi wa Rais Magufuli Kununua Ndege Badala ya Kutoa Huduma Kwa Jamii, Awataka Vijana Kuwa Imara 2020
6
December 15, 2016
Tags
Mmmmmmh mimi hawa viongozi waliokuwa ×viongozi walaaa!!!!. Kwa sababu walikuwa viongozi na walaaa awakufanya hayo wanayoyaongea tena watafanyaa sasa. Mmmmh hapa tusidanganyanye. Wote uwaribifu wa nchi ni kutokana na matunda waliyoyapandikiza huko nyuma. Huduma mbaya za afya. Miundo mbinu mibovu. Kupolomoka kwa elimu. Kukosa hata raslimali za serikali kama Huduma za usafirishaj. Wa anga ama barara. Mmmmh huyu baba awadanyanye hao wenye kudanganyika. Hamna vision. Wala focus yoyete hapo. Wawachie wapya wapeleke mbele gurudumu la Taifa. Mambo hawa hayarudi nyuma Bali yanasonga mbele nae wakati wake wa Uongozi ulisha ishia. Kwa kujaribu aweza jaribu kutafuta huo Uongozi. Uongozi si lelemama katika ulimwengu wa sasa kila kitu kiko wazi. Na asilimia kubwa ya wafrica wameshachoka na viongozi bla bla. Asa bara la Africa. Watu wamechoka kudhalauliwa na kuitwa watu wa dunia ya tatu. Sub Sahara. Sub human. Watataka viongozi wa kweli. Sio wanaowaza kujitajisha wao na familia zao na makundi yao na jamaa zao. Mambo haya yako asa huku kwetu bara jeusi.
ReplyDeleteAcha maneno uza mifugo uchangie maendeleo tukuone
ReplyDeleteNenda kajinyeeee huko usituletee ujinga wako hapa. Mtu mwenyewe umeishiiiiwaaaaaa
ReplyDeleteHapana,maneno machafu ya nini hata kama ilitokea?huu sio uungwana,kwa mtu mwenye hekima unaweza kutumia maneno ya busara kupeleka hisia zako kwa mlengwa lakini sio haya maneno uliyoandoka,haifai hata kama ndio uhuru wa kuandika.Heshimu kila mtu hasa wakubwa.
Deletekweli kabisa
DeleteHuwa nashangaa sana kiongozi kama Lowasa anapoiponda serikali ya Magufuli,hivi si na wewe ulikuwa kwenye kundi hilo kabla hawajakuengua?mbona hukuwa unakemea mabaya yaliyokuwepo?Mbaya zaidi kwa hela ulizo nazo basi kama kweli una nia njema na hao wananchi ungesaidia hata kuchimba visima huko umasaaini kwenu mahali ambako maji bado ni shida,yaani ningekuunga mkono kwa asilimia zote.Sijui kwa nini siwaamini,naona kama mnayoongoa ni kama kupamba walala hoi kwa lengo la kufanya waichukie serikali na kama sio uroho wa madaraka.Yaani mtu kama Bashe kesho akihamia upinzani na kuendelea kuikosoa serikali nitamuunga mkono lakini wewe sikuamini kabisa.
ReplyDelete