Mji wa Moshi umekuwa na msongamano mkubwa wa magari katika barabara kuu ya kuingia mjini kutokea Dar es Salaam.
Msongamano huo wa ongezeko la magari unalosababishwa na utamaduni wa wenyeji wa Mkoa Kilimanjaro, kurejea nyumbani kutokea mikoa mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Awali, ilitarajiwa kusingekuwapo na ongezeko hilo la wageni kwa mwaka huu, kutokana na ugumu wa maisha uliotokana na kupungua kwa mzunguko wa fedha mitaani.
Hata hivyo, juzi saa 12.00 jioni hadi saa 2.00 usiku, kuliibuka msongamano wa magari kuanzia eneo la Mbwaharuki hadi Magereza Barabara Kuu ya Dar es Salaam- Moshi.