MAONI: Kwa Mujibu wa Vigezo vya EATV Awards, Alikiba Anastahili Tuzo 3 Alizopata

Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa muziki wa Tanzania na kwa jicho ziada, nimezifuatilia kwa kina tuzo za EATV zilizofikia kilele jana. Nimeona, kuna kuna watu wanalalamika pasipo kujua utaratibu wa tuzo hizi ukoje. Ili kuwa nominated kwenye EATV Awards, ilikuwa ni lazima kwanza msanii achukue fomu ya ushiriki ndipo aweze kuingizwa katika orodha ya wasanii watakaoshiriki.


Jopo la EATV likafanya mchujo kupata orodha ya watu 5 ambao watapigiwa kura.

Sifahamu vigezo vyao katika kuchagua nyimbo zilizostahili kuingia katika 5 bora kwa kila kipengele, lakini ninachojua ni kuwa nyimbo zote au wasanii waliopita kwenye 5 bora wamestahili kabisa. Ukipitia habari hii, Hawa ni washindi wa tuzo za EATV 2016, Alikiba akomba tuzo 3, utagundua kuwa kuna baadhi ya watu wanalalamika kuhusu Video bora ya mwaka.

Naweza kusema labda ni kwa sababu ya hizi Team fulani na Team fulani.

Ebu tafakari kidogo kwanza. Nini maana ya kupiga kura? Ukitazama orodha ya video 5 zilizoingia, nadhani hakuna ubishi kuwa AJE ya Alikiba imefanya vizuri kushinda video zote zilizoshindanishwa naye katika kipengele cha video bora.

Achilia mbali kura alizopata Alikiba na kumfanya kuwa mshindi wa video bora, bali msanii huyu ana hazina kubwa sana ya mashabiki na wanakesha wakimpigia kura.

Tazama kidogo washiriki wa kipengele hiki:

1. Alikiba – Aje
2. Shetta – Namjua
3. Navio – Njogereza
4. Joh Makini – Dont Bother
5. Lady Jaydee – Ndi ndi ndi

Hata kwa upeo mdogo tu, kinyang’anyiro cha kipengele hiki kilikuwa ni cha watu watatu Alikiba, Joh Makini, na Lady Jaydee, ” maana kwa haraka haraka tu ndio wenye nguvu zaidi kwa Tanzania.

Hivyo kwa mtazamo wangu, Alikiba amestahili kabisa kuchukua tuzo tatu alizo pata hapo jana. Hongera sana kwa EATV kwa kuweka alama katika tasnia ya burudani Tanzania. Bila shaka tutarajie mengi zaidi mwakani maana ninaamini huu ni mwanzo tu na ni mwanzo mzuri kabisa.

Napenda niaache kwa maneno haya tu, “Tuache maneno, tuwasapoti wasanii wetu wanaofanya muziki mzuri.”

Imeandikwa na Ally Msangi
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umeandika hujui vigezo vilivyo tumika, sasa unawezaje kusema mtu anastahili au hastahili bila kujua vigezo? Je unajua vigezo vilivyotumika kuchuja hayo majina na kuishia kwenye hio list?

    ReplyDelete
  2. to frank with you guys even mimi ni nafatilia vizuri muziki wa tanzania bongo fleva ukweli haufichiki na siku zote suo jumapili what i am trying to say is Kiba ameahinda na diamond hakuwa kwenye list so vp diamond anaingizwa hapo kuweni wa kweli Kiba aneshinda na ataendelea kushinda he is amazing iblove his songs sauti yake tofauti kabisa huwezi kumlinganisha na diamond keep it up King wenye wivu wajinyonge

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad