MKULIMA Aliyechomwa Mkuki na Wafugaji Apata Nafuu Baada ya Mkuki Kutolewa

Maendeleo Ya Ndugu AUGUSTINO MTITU aliyejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki jana tarehe 25/12/2016 Kijiji cha Dodoma Isanga Kata Ya Masanze Jimbo La Mikumi na jamii ya wafugaji, hivi sasa anaendelea vizuri na matibabu baada ya kutolewa mkuki mdomoni salama salimini kwenye HOSPITALI YA MKOA MOROGORO na amelazwa wodi namba moja hospitalini hapo.

Ofisi Ya Mbunge Jimbo La Mikumi inatoa shukrani zake za dhati kwa Madaktari na wauguzi waliofanikisha zoezi hilo, Lakini pia Ofisi Ya Mbunge Mikumi itakuwa ikiwapa maendeleo ya Bwana AUGUSTINO MTITU mpaka hapo hali yake itakapokua imetengemaa.

Lakini la muhimu zaidi Mh. Mbunge amefanya mawasiliano na ngazi mbalimbali zinazohusika akiwemo Waziri wa Mambo Ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba juu ya kile kilichotokea na waziri amesikitika sana na ameahidi kulifuatilia suala hili kwa kina na kulitolea maamuzi magumu.

Imetolewa na :- Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Jimbo La Mikumi

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. inatia huruma jamani pole sana Mungu ni mkubwa umetibiwa na utapona tu mwenyezi Mungu yupo na wewe, na hao walikufanyia hivyo watakamatwa tu na watachukuliwa hatua kali za kisheria

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad