MR Nice Afunguka Haya Baada ya Kuzushiwa Amefariki Dunia.....

Msanii mkongwe wa muziki, Mr Nice amesikitishwa na watu ambao wamemzushia kifo katika mtandao wa kijamii.


Mtandao mmoja wa kijamii uliandika taarifa za uongo kwamba muimbaji huyo amefariki akiwa nchini Tanzania.

Mr Nice ambaye yupo nchini Kenya amesema alishangaa kuona watu wakimpigiwa simu kwa nyingi na kuulizwa kuhusu afya yake na alivyofuatilia akagundua kuna mtandao umeandika taarifa za uongo kwamba amefariki.

Kupitia facebook, Mr Nice aliamua kuandika taarifa hii:

East africa vibes nawashukuruni sana kwa kunizushia kifo sina la kuwajibu ,,ila mungu awalipe kadri ya vile mnavyostaili kwa hiki mlichonizushia leo ….mungu ni wetu sote na hasikilizi amri za binadamu so atakaponihitaji ataniita kwa mapenzi yake but si nyie east african vibes mnaoweza kuniua wala yeyote yule chini ya hili jua …kama nyie hamuioni thamani yangu hilo ni juu yenu kwani huku niliko mimi ni kama lulu na maisha yanaendelea tena kwa kiwango cha juu kabisa ..hii si mara ya kwanza kunizushia kifo na mambo mengine ya ajabu ajabu ila all in all mi nipo na bado mtaniona sana nikiendelea kuwepo ….im total dissapointed kwakweli …mungu awape stahiki yenu ..THANKS SANA EATV 13/12/2016
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. me nafikir kama una ushahid kamili nadhan una haki ya kulipeleka suala hilo kwenye hatua za kisheria..au kama nmekosea kufikir bas mwachie Mungu tu.

    ReplyDelete
  2. kwa kweli wabongo ni watu wabaya yaani mnabandika mitandaoni picha za zamani kipindi alikuwa anaumwa halafu mnamzushia kifo kila mtu huwa anaumwa katika maisha ndiyo kweli kuna kipindi aliumwa lakini ni zamani na alishapona lakini bado tu mnaendelea kuandika kutoka kipindi kile mpaka leo kwani nyie hamjawahi kuumwa katika maisha yenu? jamaa mpaka akaamua kuhama nchi kuweka makazi yake nchini Kenya ambako bado wanamkubali lakini nyie bado tu mnamtakia mabaya nyie watanzania kama mlimchoka basi mwacheni aendelee na maisha yake nchini kenya ambako anapojitaftia riziki, chuki za nini? du wabongo ni balaa chuki na roho mbaya ni zenu hamna lolote la kufanya kazi zenu ni kukalisha mitako na kuongea majungu mitandaoni kila kukicha na Mr Nice kawajibu vizuri sana na amewapatia. Big up Mr Nice, enzi za zamani wakati anavuma mlimpenda sana mlikuwa mnapiga mziki Wake kila kona leo hii mnamuona hafai ama kweli nyie wabongo kuna ile kauli wanayosema tenda wema nenda zako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad