MSHIRIKI wa Bongo Star Search Aeleza Sababu ya Washindi Kushindwa Kufanya Vizuri Sokoni

Hadi sasa watu wanajiuliza nini kimetokea kwa Kayumba – mshindi wa Bongo Star Search mwaka jana. Mbona kijana huyo alionesha uwezo mkubwa wakati wa shindano hilo kiasi ambacho walimtabiria angekuja kuwa kuwa Diamond wa pili?

Alitoa wimbo ambao video yake ilifanyika nchini Afrika Kusini lakini haukuweza kufanya vizuri. Na sasa jina lake limesahaulika kabisa. Tatizo liko wapi? Mshiriki wa shindano hilo ameeleza maoni yake kwenye comment za post niliyoweka wiki kadhaa zilizopita kuhusiana na wimbo wa gospel wa Walter Chilambo ambaye aliwahi kushinda taji la BSS.

“Katika harakati za kutafuta majibu ya kwa nini washindi wa BSS hawafanyi vizuri kwanza nitakujibu kama mdau wa muziki, pili kama mshiriki wa EBSS 2012 pekee kutoka Mwanza aliyetolewa katika Top 09,” anasema.

“Kwanza tatizo kubwa la BSS ni kutopromote ubunifu. Haiwajengi washiriki wake katika kujitegemea kwenye utunzi na uimbaji. Shindano limebase kwenye kuimba covers, na hapa naenda mbali zaidi cover zinatakiwa ziimbwe kama original songs, no improvision sababu ukifanya hivyo utaonekana haujautendea haki wimbo.”

Ameendelea, “Pili, washiriki na hata ma judge wanawaza sana kuhusu ile million 50 itaenda kwa nani kuliko kuwaza katika ni mshiriki gani atakuwa brand mpya ya music na anaweza kusimama na kuuteka umma kwa performance, hili hupelekea kutumia kigezo kimoja tu kumpa mtu ushindi.

Tatu, ni management. Washindi wengi wanakosa management za uhakika sababu mara baada ya shindano kuisha tu, biashara inafungwa na msanii anaachwa akajitegemee. Na hapa hata kama utaona ana management ujue ni kwa muda tu kipindi ambacho hali yake kiuchumi inapokuwa nzuri. Baada ya hapo msanii huyo atarudi kuwa hovyo pengine hata zaidi ya alivyokuwa kabla hajaingia Lamborghini.”

“Nne ni elimu,” anaendelea. “Ni ukweli mchungu ila tuumeze tu ili tujifunze. Washiriki wengi wa BSS ni vijana wadogo sana kiumri na kielimu pia. Na wengi wao hutoka katika familia zenye kipato kidogo. Kwa hiyo wanapoingia mle kwenye shindano kwanza wanaona kama bahati. Pili nafasi pekee ya kijikwamua, tatu wanakuwa hawatambui haki zao na kubwa zaidi wanakuwa hawajajiandaa kuupokea u star. Ndio maana wengi wao kama sio wote hawawezi kusimama peke yao mara baada ya mashindano. Na wengine wakishaupata u star, kutokana na kukosa elimu ya kutosha kunawafanya wanakuwa malimbukeni hivyo kuishia kuharibu vipaji vyao.”

“La mwisho, Judges wajenge a fair platform kwa washiriki wote ili kupata washindi wa kweli, mihemko ipungue, wasitake sides, na wasiwe na personal interest kwa washiriki ili kupata mshindi wa kweli. Amini nakwambia katika most of the time, the best singers never win competition. Kwa kusema hilo pengine waimbaji bora hutolewa kwa vigezo(vya kijinga) vingine tu ili majaji waonekane wana power lakini matokeo yake ndio haya tunayoyaona. Their winners never move even a baby step ahead. Ni matumaini yangu umejifunza kitu.”

Bongo5
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad