Miongoni mwa sifa kuu za ziada na za pekee za rais wetu Mhe. Dr John Pombe Joseph Magufuli, ni sifa ya kuwa mkweli daima toka ndani ya nafsi yake. Linapokuja suala la kuusema ukweli, Magufuli yuko very bold, atausema ukweli no matter what.
Taifa hili limefika hapa tulipofika kwa viongozi kuogopa kusema ukweli na badala yake kuuremba remba au hata ikibidi kusema uongo ili tuu kuwafurahisha watu lakini Magufuli kwenye hii falsafa yake ya hapa Kazi tuu, ni mwendo wa mchaka mchaka katika ukweli na uwazi.
Hivyo wanapojitokeza watu wakweli na wawazi kama alivyo rais Magufuli ambao ni watu ma bold wenye guts za kusema ukweli no matter what, watu hawa ni mashujaa wa taifa hili, miongoni mwa mashujaa hawa, ni aliyekuwa Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru, ambaye kutokana na kuwa mkweli too much, amepumzishwa na kusubiri kupangiwa kazi nyingine muhimu zaidi kuliko Msajili wa Hazina.
Ukweli aliousema Mafuru, ni kuwasaidia Watanzania kumwelewa vizuri zaidi rais wao, alipotoa amri ya fedha za umma kutunzwa BOT pekee, watu hawakunwelewa rais, wakadhani rais amepiga marufuku taasisi za umma kutumia mabenki binafsi, kumbe rais alimaanisha ni fedha tuu za makusanyo ndizo zinatunzwa BOT, lakini fedha za matumizi zonaendelea kuwekwa mabenki binafsi na hakuna ubaya wowote kuzifungulia Fixed Deposits.
Kuondolewa kwa Mafuru, kunatafsiriwa na wengi kuwa ni kutumbuliwa, kumbe wengi hawajui, kule sio kutumbuliwa bali ni kuandaliwa kwa majukumu mengine makubwa zaidi.
Haiwezekani mtu ufanye kitendo cha ushujaa kama kuwasaidia wananchi kumwelewa vizuri rais wao badala ya kupongezwa badala yake ukatumbuliwa, nasisitiza Mafuru ni shujaa na anastahili kupangiwa majukumu mengine muhimu zaidi. Swali ni Jee Mafuru atapangiwa jukumu gani muhimu?.
Shujaa mwingine kwenye hili la mambo ya fedha na uchumi ni Gavana wa Benki Kuu, Prof Beno Ndulu ambaye na yeye alilifafanua.
Nampongeza Lawrence Mafuru na kumtakia maandalizi mema ya kusubiri kupangiwa kazi nyingine.
Paskali.
I beg to differ. Kama nia ni kumpangia majukumu mengine, kwa kawaida unamhamisha mtu kutoka jukumu flani, na straight unmuweka kwenye jukumu hilo lingine. hayamambo ya "ku pumzishana kwanza" wakati unasubiri kupangiwa jukumu lingine wengine tunayachukulia sio mazuri sana.
ReplyDeleteNa pia pamoja na sifa ulizozitaja za rais wetu, umeisahau nyingine muhimu;
Huwa hapendi sana mtu mwnye mawazo yanayokinzana na ya kwake, hata kama mtu huyo atakuwa yuko sahihi kuliko yeye. Style hii ya utawala/oungozi ilikua inatumika karne ya 15,16 mpaka 18.
😃😃😃😃😃
DeleteHiyo Allocation inayopelekwa kwenye Taasisi mbalimbali za Serikali zinatakiwa kuwa revolving funds. Kwa maana ya Fedha zinazoingia katika expenditures mbalimbali za hizo Taasisi kwa maana ya kila siku moaka mwezi na miezi. Sasa unapoiweke kwenye hiyo Fixed Deposit Account maana yake ni nini. Na hizo taasisi zinapata wapi fedha nyingine zaidi ya zile zilizokuwa Allocated kwao kwa ajili ya expenditures za kila siku mpaka mwezi na miezi??????......Huo ni uhuni wa hali ya juu sana wa baadhi ya maofisa wasiokuwa waaminifu wa hizo taasisi za Serikali. Unapoweka Fedha kwenye Fixed Deposit Account maana yake ni kuwa haiguswi na lengo likiwa ni ku generate interest. Sasa hao maofisa wa Serikali wanapofanya maamuzi kama hayo ni kwa faida ya nani. Na je zile interest ambazo zinakuwa generated based na hizo fedha zinaelekezwa wapi. Je wanachokifanya ni kwa mujibu wa government financial circular ama ni zile internal decisions ambazo zinafikiwa na maofisa wachache ambao sio waaminifu kwa manufaaa yao??????......Wasitake kutufanya sisi Watanzania ni wajinga. Hao maofisa wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda mrefu kwa kuitumia hiyo fursa na kujipatia faida huku wale walengwa na hasa wafanyakazi wa chini wa hizo taasisi wakibakia kutaaabika.
ReplyDeleteHawa ni aina ya wale maofisa wa Serikali ambao wamekuwa wakizifuja vibaya hela za Walipa Kodi. Na ndio maana ukitembelea majengo mbalimbali ya taasisi za Serikali unakuta yamechakaaaa na hayo katika hali nzuri. Kuanzia Rangi ya Jengo mpaka viti vya kukalia wageni sehemu ya mapokezi. Na pia imekuwa ni jambo la kawaida kukuta kwenye ofisi za taasisi mbalimbali za Serikali hazina viyoyozi na vyoo. Na hasa zile ofisi zilizopo Dar es Salaam. Lakini haya yote ni mambo yanayosababishwa na aina ya hawa viongozi wafujaji wa fedha za Serikali. Badala ya kuzitumia zile fedha walizopangiwa kuendeleza zile shughuli za taasisi zao ikiwamo kuyakarabati majengo yao na kuyafanya yaonekane nadhifu. Badala yake wao wanazichukua zile fedha na kuzikalia kwa kuziweka kwenye fixed deposit accounts kwenye Ma Bank mbalimbali.Kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa Serikali.
ReplyDelete"Huwa hapendi sana mtu mwnye mawazo yanayokinzana na ya kwake, hata kama mtu huyo atakuwa yuko sahihi kuliko yeye.".............unataka akubaliane na kila mawazo ya mtu ambayo ni sahihi katika kupiga dili na kula rushwa pamoja na ubadhirifu mwingine wa mali za umma. Huyu ni Rais aliyewaambia Watanzania kutoka mwanzo kuwa ni mtu anayechukia hizo dili zenu ambazo zimelifikisha hili Taifa hapo lilipo.
ReplyDeleteReasoned opinion leads to failure to comply.
ReplyDeleteInfringement case as opposed to Domestic law in compliance.
ReplyDelete