Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo (Alhamisi) amemwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo, Kisale Makori na kumtaka kutokaa ofisini na kusubiri taarifa badala yake atoke nje na kusikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo.
Makonda amesema changamoto kubwa ya watendaji ni uwajibaki na kwamba baadhi yao hupenda kusubiri kupelekewa taarifa za wananchi ofisini badala ya kuwafuata wananchi katika maeneo yao.
"Naomba Makori usiwe mtu wa kusubiri taarifa ofisini pekee.Wanaubungo wanamatumaini makubwa na wewe kwa sababu umeaminiwa na Rais (John Magufuli),"amesema Makonda.
PAUL Makonda Amtaka DC wa Ubungo Kufuata Nyayo zake
1
December 23, 2016
Tags
Mungi akubarikini viongozi wote wenye Nia njema na nchi na wananchi. Uzelendo wenu na mapenzi yenu katika kututimikia sisi wananchi kwa Uaminifu na uadilifu...Mmuungu atakupeni malipo yake. Na kukuzidiahieni Afya njema na umuri tawile..Hapa kazi Tu. Kazi zetu na uwajibikaji wewe Ni wa kuigwa. Makonda na timu yako mabadiliko tunayaona
ReplyDelete