Mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote leo alipokuwatana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini.
Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema leo meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake itawasili nchini. Ameongeza kuwa lengo la kufanyabiashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.
Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 imetia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo.
Aidha, imeelezwa kuwa wiki ijayo meli nyingine kutoka Korea Kusini yenye malori 451 inatrajiwa kuwasili katika bandari ya mkoani Mtwara.
Ahaji Aliko Dangote. Kwa Imani yako na Katika kumuenzi Allah. Umeona unawajibika kuendeleza na kuwatafutia Ajiria ndugu zako waliopo Tanzania. Dhana Hii ni Nzuri na tuaipenda Inshaalaah hapa hauto Dhulumiwa. Na tutahakikisha Chako cha Halali unapata Na chetu stahiki tunapata. Win Win situation on Both Parties. We thank you for What you AIM on. and will cooperate with you for the benefit of our / your Business Develpoment. Though competition and quality rules the Day. We are there for you. Hapa Kazi Tu
ReplyDeleteAhaji Aliko Dangote. Kwa Imani yako na Katika kumuenzi Allah. Umeona unawajibika kuendeleza na kuwatafutia Ajiria ndugu zako waliopo Tanzania. Dhana Hii ni Nzuri na tuaipenda Inshaalaah hapa hauto Dhulumiwa. Na tutahakikisha Chako cha Halali unapata Na chetu stahiki tunapata. Win Win situation on Both Parties. We thank you for What you AIM on. and will cooperate with you for the benefit of our / your Business Develpoment. Though competition and quality rules the Day. We are there for you. Hapa Kazi Tu
ReplyDeleteAllah anampa mwenye roho safi.
ReplyDelete