POLISI Wapigwa Marufuku Kuvisha Mabango Madereva Walevi

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema wamesitisha kuwatangaza watuhumiwa katika mitandao ya kijamii  baada ya kupata malalamiko ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Hata hivyo, amesema hadi wanasitisha walikuwa wamewakamata  madereva 20 wa Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuonyesha jamii ili wengine wenye tabia hiyo wajifunze kupitia kwa wenzao na kuacha kuendesha wakiwa wamelewa.

“Kwa sababu watu wengi wapo mtandaoni ilikuwa rahisi ujumbe kuwafikia kwa wakati mmoja. Tulipata malalamiko ya haki za binadamu kuwa kufanya hivyo kunawasababishia kudhalilika katika familia zao, tukaona tusitishe,” amesema Mpinga.

Hata hivyo, amesema pamoja na kusitisha utaratibu huo, madereva wasijisahau kwa sababu vijana wapo kazini na wanaendelea kuwakamata wale wote watakaokiuka sheria za barabarani, ikiwamo hiyo ya kuendesha wakiwa wamelewa.

Awali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imelitaka Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, kuacha kuziweka hadharani picha za madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria, badala yake liwafikishe mahakamani kwanza.

Kauli ya Tume hiyo imetokana na utaratibu ulioanzishwa na trafiki wa kuwavisha mabango madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria ambayo yameandikwa makosa yao na kurushwa kwenye mitandao ya kijamii kabla hawajafikishwa mahakamani.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga amesema hayo wakati akifafanua kuhusu kusitisha kuwaanika katika mitandao ya kijamii madereva wanaokamatwa na trafiki kwa makosa ya usalama barabarani ikiwamo ulevi

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inaelekea hao wanaojiita haki za binadamu wenyewe pia ni walevi ndio maana wanatetea walevi wenzao...., yaani wanajali haki za walevi kuliko kuangalia athari zinazo sababishwa na huo ulevi!! Kunawatu wameacha kunywa pombe kuogopa kutangazwa, Polisi hebu rudisheni bana, achaneni na hao wanaojiita eti haki za binadamu .....Kwa kweli binafsi hawa watu wanaojiita haki za binadamu,sielewi kazi zao hasa ni zipi??? Watoto wakibakwa huwasikii, ma'dada wa kazi na watoto wadogo wanateswa huwasikii, polisi wakipigwa na wananchi huwasikii, vituo vya polisi vikichomwa moto huwasikii, hata yule mwanafunzi wa Mbeya alopigwa na walimu watano kama kibaka,hawakusema chochote.......wanangoja maandamano yapigwe marufuku, walevi wavishwe mabango, na mengine yasiyo na kichwa wala miguu utaona jinsi povu linavyo watoka kwa kutetea...hovyoooo. Ni heri wangefutiliwa mbali.....siwapendi mfyuuuuu

    ReplyDelete
  2. Kama hawataki kutangazwa waache kuendesha wakiwa wamelewa, hayo ya kuwatangaza yanafanyika kwa faida yao pia

    ReplyDelete
  3. Hapa haki ya dereva mlevi imepewa kipaumbele kuliko ya haki ya kushi ya atakaegongwa na gari la dereva mlevi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad