POLISI Yaomba Msaada Kumtafuta Msaidizi wa Mbowe

Baada ya kukaa siku 33 bila kuzungumzia kutoweka kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, jana Jeshi la Polisi lilijitokeza na kuomba msaada kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.

Aidha, hatua hiyo ya Jeshi la Polisi imetolewa wiki moja tangu Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu atoe tamko la kuitaka Serikali kueleza kama imemkamata au inamshikilia kada huyo aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 18.

Mbali ya kutaka Serikali ieleze mahali alipo msaidizi huyo wa Mbowe, pia mwanasheria huyo alitaka ufuatiliwe ujumbe wa vitisho aliowahi kutumiwa kupitia simu yake ya mkononi na mtu asiyejulikana.


Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Siku nne baada ya Ben kupotea au kutoonekana ndio taarifa zikaanza kutolewa,kwa nini?Kupotea kunaripotiwa baada ya masaa 24,kwa nini kwa Ben ni zaidi ya muda?Ujumbe wa vitisho vya mtu asiyejulikana ulikuwa lini au umechukua muda gani mpaka Ben kupotea?kwa nini huo ujumbe usingeripotiwa mapema mpaka Ben apotee ndio tunasikia kwamba kulikuwa na ujumbe wa kumtishia Ben?Mmmmh,muogopeni MUNGU jamani.Hapo Kuna kitu.

    ReplyDelete
  2. Mbowe aulizwe msaidizi wake yuko wapi? Mara ya mwisho alionekana wapi na saa ngapi na nani?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad