Hadi inafika saa saba usiku mwanamuziki hiyo hakuwepo ukumbini alipotakiwa kuanza kutumbuiza saa nne. Baadhi ya watu waliokuwa ndani ya ukumbi walianza kuleta vurugu na kudai fedha zao ili waondoke kwani muda ulikuwa umekwenda sana.
Akizungumza, mtayarishaji wa tamasha hilo Rashid Adam maarufu Chidi Perugina alisema tatizo kubwa lilikuwa ni suala la usafiri ambapo Ali Kiba alichelewa kufika mkoani Dodoma.
Ali Kiba alikuwa Nairobi na alitegema apande ndege awahi kufika Dar es Salaam na kisha aanze safari ya kuja Dodoma, lakini tatizo lilitokea baada ya Ali Kiba kukosa ndege ya kwanza aliyotakiwa kutoka nayo Nairobi. Ndege ya pili aliyopanda ilichelewa kufika Dar es Salaam na kuanza mchakato wa safari ya kufika Dodoma ulisababisha Ali Kiba kufika hapa saa saba usiku na madakika, alisema Rashid Adam.
Baada ya Ali Kiba kufika aliwaomba radhi mashabiki wake wachache waliokuwa bado wapo ukumbini na hakuweza kutumbuiza sababu ya uchache wao.
Baada ya tamasha hilo kusindwa kufanyika hiyo tarehe 25 Disemba, Ali Kiba anatarajiwa kutumbuiza terehe 28, Januari 2017 ambapo mashabiki walio na tiketi wametakiwa kuzitunza ili kuzitumia kwenye tamasha hilo lingine. Angalia Video:
Mwanamuziki @OfficialAliKiba ashindwa kutumbuiza katika tamasha la muziki, Dodoma Disemba 25 baada ya kufika kwa kuchelewa akitokea Nairobi. pic.twitter.com/SnDkrsGDwU— Swahili Times (@swahilitimes) December 27, 2016