WASANII Watano Matajiri Kupita Wote Afrika Watajwa..Mtanzania Mmoja Yupo Kwenye List

Mara nyingi tumezoea kuona list za wasanii wakubwa wakitajwa kuingiza pesa nyingi zaidi Afrika, wiki hii imetoka list iliyoandikwa na eDaily kupitia ripota Brian Okoth ambayo imewataja wasanii watano kutoka Afrika wanaotajwa kuingiza pesa nyingi zaidi mwaka 2016.

5. Diamond Platnumz (Tsh. Bilioni 9,665,923,190.55)

Related imageMtanzania Diamond Platnumz huenda akawa msanii anayezungumzwa au kutajwa sana kwasasa barani Afrika kutokana na headlines anazotengeneza kila siku, mikataba yake na makampuni makubwa kwenye kazi zake pia inazidi kumuweka sehemu nzuri kifedha.

Hakuna shaka kwamba Diamond ni mmoja kati ya wasanii wanaoingiza pesa nyingi kupitia muziki wao kwasasa, na hili litaondoa utata kuhusu kiasi cha pesa alichotajwa kuwanacho staa huyu wa single ya Make Me Sing ambaye aliwahi kuzungumza na E!TV Jumapili ya, June 26 mwaka huu na ikaelezwa kuwa anamiliki pesa zinazozidi kiasi cha dola Milioni Mia Nne za Marekani (Zaidi ya Bilioni 9 za Tanzania).

Kiasi hicho cha pesa hakijaja tu kama suprise kwa Diamond, ambaye anatajwa kuwa ndiye msanii anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye show au event yoyote anayotakiwa kuhudhuria nchini Tanzania na pengine Afrika Mashariki kwasasa.

Pesa nyingi zinaelezwa kuingia kupitia shows alizofanya ndani ya Tanzania, East Africa na nje ya Afrika. Diamond Platnumz pia amekuwa balozi wa makampuni mengi makubwa ya biashara ikiwemo Vodacom, Cocacola, DSTV, Uber Taxi na Red Gold.

Ziko taarifa kuwa Diamond Platnumz huchaji si chini ya shilingi milioni 25 kwa show moja ya kawaida akiwa Tanzania, pia gharama hizo hufikia shilingi milioni 50 na kuendelea akiitwa na kampuni ya biashara na kama akiitwa nje ya Tanzania basi gharama zake huanzia shilingi milioni 200 na kuendelea.

Vyanzo vingine vya mapato ni pamoja na mauzo ya miito ya simu ambayo inaelezwa hakuna msanii yeyote Afrika Mashariki anayefikia mauzo yake kwenye ukanda wa maziwa makuu, pia anamiliki akaunti ya Youtube ambayo ipo kwenye list ya chaneli 10 zinazoangaliwa zaidi barani Afrika.

Hivi karibuni Diamond Platnumz ameingia kwenye biashara za kununua nyumba za zamani na kuzifanyia ukarabati ambapo huzipangisha, kitu kinachotajwa kumuingiza mkwanja mrefu zaidi jijini Dar es salaam, mbali na kumiliki record lebel yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo kwa mujibu wake Diamond aliwahi kusema wamesaini deal ya zaidi shilingi Bilioni 2 na lebel ya Universal Music Group ya Marekani ili kusambaza kazi za wasanii walioko chini yake ambao ni Rich Mavoko, Harmonize na Rayvany.

4. Wizkid (Tsh. Bilioni 25,676,809,453.47)

Kwa mujibu wa Infoguide Nigeria, mpaka kufikia December 2015 mwimbaji star Wizkid alikuwa anakadiriwa kumiliki kiasi cha dola Milioni  11.5 ambazo mpaka mwisho wa mwaka 2016 inaelezwa kuwa amefikisha dola Milioni 12.

Wizkid amekuwa na mikataba inayomuingizia pesa nyingi na makampuni kutoka Nigeria ikiwemo label yake ya Star boy Records aliyoianzisha mwaka 2010. Pia mwaka 2014 Wizzy alisaini deal ya kuwa balozi wa kampuni ya simu ya MTN ambao walimlipa zaidi ya shilingi milioni 300 na kampuni ya MTN rival Globacom ikapanda mara mbili ili kumtumia Wizkid kama balozi wao.

Deal hiyo ya miaka miwili inatajwa kumuingiza Wizkid zaidi ya shilingi milioni 900 kutoka kampuni ya Globacom na mwaka 2015 wakati akifanya sherehe ya kutimiza miaka 25 Wizkid alisaini upya mkataba wake na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi.

Ukijumlisha kiwango cha pesa anachoingiza kutoa kwenye shows anazofanya, mauzo ya nyimbo zake, tuzo, zawadi pamoja na mikataba yake, inamuweka star huyo kwenye list wasanii wanaoingiza pesa nyingi zaidi nchini Nigeria. Zipo taarifa kuwa ili kuweza kumualika Wizkid aje kufanya show ya kampuni itakubidi umlipe si chini ya shilingi milioni 60.

Kumbuka pia mwezi August, 2015, WizKid alitajwa kwenye jarida la Forbes kama miongoni mwa mastaa 14 wanaoitangaza Afrika.

3. Davido (Tsh. Bilioni 30,502,418,406.03)

Kwa mujibu wa Nigerian Finder wameeleza kuwa Davido anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 14 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 30 za Kitanzania.

Pamoja na kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa kifedha, hiyo haikumfanya Davido kurelax badala yake alitumia nafasi yake kama msanii kujenga jina lake na kufanya biashara inayomfanya kuingiza pesa nyingi kwenye akaunti zake.

Mwaka 2012, Davido alisaini deal na kampuni ya MTN TV kama balozi na akasaini deal nyingine na MTN Pulse kuwa muwakilishi wa kampuni hizo kwa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 207 za Kitanzania, wakati huo huo mwaka 2014, Davido alilipwa zaidi ya shilingi milioni 341 kuwa balozi wa kampuni ya dawa za meno ya Close UP.

Pia Davido na kaka yake Adewale Adeleke wanamikili lebel ya muziki iitwayo HKN Music ambayo imekuwa ikiwaingiza pesa nyingi kupitia mauzo ya nyimbo za wasanii waliosaini lebel, mauzo ya albam pamoja mikataba ya matangazo.

2. Akothee (Tsh. Bilioni 132,683,540,000.00)


Huenda ikakushtua sana kutokana na jina la msanii huyu kutokua kubwa sana au kutofahamika sana kwa watu wengi, Mwimbaji Akothee kutoka Kenya anatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola za Marekani milioni 61 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 132.

Mapema mwaka huu, mitandao ya habari za mastaa nchini Kenya iliripoti kuwa star huyo wa single ya Give It To Me alikuwa anamiliki zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 8.

Akothee amekuwa akijishughulisha na biashara pamoja na kilimo huku chanzo kingine cha mapato kikitajwa kuwa ni fidia aliyolipwa kama talaka na mwanaume wa kizungu aliyeachana naye miaka kadhaa iliyopita.

1. P-Square (Tsh. Bilioni 277,752,822,639.34)




Wakiwa ni mastaa pekee kutoka Afrika kutajwa na jarida la Forbes mara mbili kwenye list ya wasanii wanaolipwa pesa nyingi zaidi Afrika, kundi la PSquare limeendelea kuweka rekodi ya kufanya shows za gharama kubwa kupita wasanii wote Afrika, huku wakipata mialiko kutoka kwa Marais wa nchi zaidi ya 5 na usisahau, mastaa hawa wanamiliki ndege binafsi.

Kwa mujibu wa jarida la watu maarufu la Forbes, mapacha hao Peter na Paul Okoye wanaounda kundia la P-Square wanamiliki utajiri wa zaidi ya dola za Marekani milioni 130 zinazotokana na mikataba ya kibiashara na makampuni mbalimbali, biashara za mafuta, mauzo ya muziki na shows wanazofanya.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nakuunga mikono mdau kweli kabisaa

    ReplyDelete
  2. Hongera mond kwa hatua higo komaaa uchukue position ya kwanza

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad