Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha.
DAR ES SALAAM: Siku chache baada
ya kutinga mahakamani kudai talaka kwa mumewe, Emmanuel Mbasha, staa wa
Gospo Bongo, Flora Mbasha anadaiwa kuchumbiwa na mwanaume aliyetajwa
kuwa ni mwenyeji wa Kahama, Sinyanga, Daud. Chanzo cha kuaminika
kimepenyeza ubuyu wa motomoto kuwa, tukio la Flora kuvishwa pete ya
uchumba lilijiri hivi karibuni baada mwanamuziki huyo wa Injili
kutofautiana
na ‘mlinzi’ wake aitwaye Peter Shelembi.
“Si unakumbuka baada yankutofautiana na
Mbasha, Flora alikuwa ‘close’ na jamaa f’lani hivi anaitwa Peter,
alikuwa akizurura naye sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwa kama mlinzi
wake, akihofia Emma (Mbasha) anaweza kumletea fujo? Sasa nasikia mama’ke
Flora alimshawishi bintiye aolewe na Daud, naye bila hiyana akakubali.
Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha na mtoto wao.
“Ilikuwa rahisi maana hata pale kanisani kwa Josephat Gwajima (Kanisa
la Ufufuo na Uzima) alipokuwa anaabudu Flora alishaasi. Akaenda zake
kuvishwa pete ya uchumba bila hata waumini wenzake kujua,” kilidai
chanzo hicho. Baada ya kuzipata ‘good news’ hizo, Wikienda lilianza kwa
kumtafuta Daud ili kumpongeza kwa kupata ‘kifaa’ na pia kujua mipango ya
harusi. Tofauti na matarajio ya Wikienda
kwamba pengine atazipokea pongezi na
kumshukuru Mungu kuianza safari ya ndoa, jamaa huyo alipokea simu, baada
ya mwandishi kujitambulisha, alikata. Wikienda lilipiga tena ili kutaka
kujiridhisha labda pengine simu ilikatika kwa bahati mbaya lakini
safari hii alipokea na kusema yeye si Daud, mwandishi amekosea namba,
akakata tena simu.
Licha ya kujiridhisha namba hizo
zinamilikiwa na Daud, Wikienda likaona isiwe kesi, likamvutia waya Flora
ili kumpongeza na kumsikia anazungumziaje safari yake hiyo mpya
anayoianza mbali na ile ya Mbasha iliyotawaliwa na ‘sarakasi’ nyingi
hadi kufikia hatua ya kuishi kama paka na panya.
Baada ya Wikienda kujitambulisha na
kumpongeza kisha kumpa ‘full mchapo’ kutoka kwa chanzo, Flora hakutaka
hata kuzipokea pongezi hizo badala yake alisema hataki kuzungumzia jambo
hilo na kushauri gazeti
hili lizungumze na mwanasheria wake.
“Jamani mimi sipo tayari kuzungumzia chochote zaidizaidi kama mnataka niwape namba ya mwanasheria wangu,” alisema Flora.
Flora alimtumia mwandishi wetu namba ya
mtu aliyedai ni mwanasheria wake lakini alipopigiwa simu alisema kuwa,
kuna kazi anafanya, apigiwe baada ya muda. Hata hivyo, baadaye simu yake
ilipopigwa, haikupatikana hewani. Flora aliishi kwenye ndoa na Mbasha
kwa zaidi ya miaka kumi na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, Elizabeth
kisha mwaka 2015 walitengana kutokana na ugomvi wao uliofukuta chini kwa
chini kwa muda mrefu na kuibuka hadharani baada ya Mbasha kupata msala
wa kudaiwa kumbaka mdogo wa Flora. Hata hivyo, kesi iliunguruma kwa muda
na baadaye Mbasha alishinda na kuachiwa huru.
Na huyo jamaa mpya asije akasingiziwa kuwa amebaka maana huyo flora ndiyo zake hizo
ReplyDelete