Sakata la Mgogoro wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es salaam, linazidi kuchukua sura mpya,kufuatia Askofu wa Dayosisi hiyo,Dokta Valentino Mokiwa,kugoma kujiuzulu na kustaafishwa kwa manufaa ya Kanisa hilo kama alivyotakiwa na Mhasham Askofu wa Jimbo kuu la Tanzania,Dokta Jacob Erasto Chimeledya.
Hatua ya Dokta Mokiwa,kutakiwa kufanya hivyo,ni agizo la nyumba ya maaskofu la kuundwa tume ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,kuchunguza tuhuma kumi zilizokuwa zinamkabili Dokta Mokiwa,pamoja na nyinginezo, za ukosefu wa maadili,ikiwemo kufuja mali za kanisa na kuingia mikataba kiholela yenye viashiria vya rushwa katika maeneo ya Buza,ikiwemo pia kutoa daraja la Ushemasi,Upadre,na Ukanon,kwa katibu wa Dayosisi,Mkristo ambaye ametengana na mkewe na kuoa mke mwingine kiserikali kinyume na kanuni ya kanisa kuhusu ndoa.
Waandishi wa Channel Ten,wamefika katika nyumba zinazodaiwa kutelekezwa na Dokta Mokiwa ikiwemo Silver Oak ya Upanga,na ya Mtaa wa Uganda Ostabei, ambapo imedaiwa kuwa ameiacha na kwenda kupanga huku kanisa likimlipa pango la shilingi milioni 3 kwa mwezi miaka zaidi ya miaka sita.
Dokta Mokiwa jana aligoma kupokea barua yake kutoka kwa Dokta Jacob Erasto Chimeledya,na baadhi ya waamini wa kanisa hilo katika nyakati tofauti,wamezungumzia hatua ya kutakiwa kujiuzulu na kustaafishwa Dokta Mokiwa.
Katika hatua nyingine,Dokta Valentino Leonard Mokiwa,kupitia kwa Afisa habari wake,Yohana Sanha,amedai kuwa mchakato uliotumika kumuhukumu ni batili na kwamba bado yeye ni Mkuu wa Dayosisi ya Dar es salaam.