Kiongozi wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka na amesema anaondoka nchini humo kwenda kuishi uhamishoni.
Taarifa
za kuondoka kwa kiongozi huyo aliyetawala Gambia kwa miaka 22
zimetolewa na rais anayetambuliwa na jamii ya kimataifa Adama Barrow
kupitia mtandao wake wa Twitter.
Barrow ametangaza hayo baada ya mazungumzo ya saa kadha yaliyonuiwa kumshawishi Jammeh kukubali matokeo ya uchaguzi.
Mataifa
ya Afrika Magharibi yamewatuma wanajeshi Gambia na kutishia kumuondoa
Jammeh madarakani kwa nguvu iwapo angekaidi amri ya kuachia madaraka kwa
hiari.
Barrow
amekuwa nchini Senegal kwa takriban wiki moja. Aliapishwa kuwa rais
mpya wa Gambia katika ubalozi wa Gambia mjini Dakar Alhamisi iliyopita.
Ametambuliwa na jamii ya kimataifa kama kiongozi mpya wa Gambia.