Rais John Magufuli amemteua Profesa Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania.
Profesa Juma amechukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu Mohamed Chande aliyestaafu.
Kabla ya kuteuliwa katika nafasi hiyo, Profesa Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa uteuzi huo unaanza mara moja.
“Profesa Juma atakaimu nafasi hiyo hadi Rais Magufuli atakapofanya uteuzi wa Jaji Mkuu wa Tanzania,” inaeleza taarifa hiyo.
Jaji
Mkuu mstaafu Chande hadi kufikia Januari Mosi mwaka huu, alikuwa
ameshafikisha miaka 65 ambayo ni ya kustaafu majaji wa Mahakama ya
Rufani kama ulivyobainishwa katika Ibara ya 120 ya Katiba ya 1977.
Jaji
Chande aliteuliwa katika nafasi hiyo na Rais mstaafu Jakaya Kikwete
mwaka 2010 akichukua nafasi ya Jaji mstaafu Augustino Ramadhani.