Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Juma Maganga amepewa siku saba kueleza sababu ya kupitisha bajeti ya mwaka 2017/18 ikidaiwa ni kinyume na utaratibu.
Wakizungumza na waandishi wa habari, madiwani kutoka Chadema walidai kuwa mwenyekiti huyo alitumia mabavu kupitisha bajeti ambayo haijakamilika.
Katibu wa madiwani hao, Medas Amosi alisema: “Mwenyekiti alienda kinyume na kifungu cha 183 cha Sheria namba 7, na kifungu 97 cha Sheria namba 8 ya mwaka 1982 zinazotoa madaraka na mamlaka kwa Serikali za Mitaa.”
Amosi alisema utaratibu unaotumika kupitisha bajeti ni theluthi ya wajumbe ambao huwa 12, lakini mwenyekiti huyo aliipitisha baada ya wajumbe 10 ambao ni wa CCM kuikubali, huku wanane wa Chadema wakiikataa.