Kulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri tu pale Dar es salaam.
Walikuwa wakisali kanisa moja la kilokole. Mwanaume alikuwa na tabia
ya kulala usingizi kila akiingia ibadani.
Siku moja mke wake akagundua
dawa ya kumfanya jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala kanisani.
Unajua ni dawa gani hiyo?
Kukiwa tu ndo ibada imeanza, jamaa alianza kuuchapa usingizi na mke bila kukawia akamminya kwa haraka akamwambia,
Mke: “Mchungaji amekuteua ufunge ibada kwa maombi”
Mwanaume akasimama haraka na kuanza kushusha maombi makali ya kufunga ibada
Mume:“Baba katika jina la Yesu tunakushukuru kwa ibada nzuri, Asante kwa
ujumbe wa leo kutoka kwa mtumishi wako Mchungaji, Asante kwa miujiza ya
uponyaji. Tunaomba ututangulie tunapokwenda majumbani kwetu kupumzika,
Kanisa woote tuseme Amen”
HAKUNA ALIYESEMA AMEN badala yake baada ya kumaliza sala tu,
alilishuhudia kanisa nzima likimkodolea macho huku wengine wakicheka
sana, na wengine wakiwa midomo wazi na wengine wakiinama kwa aibu kwani
ibada ndo tu ilikuwa imeanza na jamaa anashusha sala ya kufunga ibada!
Nimesikia kuwa huyo bwana aliacha hiyo tabia ya kulala lakini sikujua mahusiano yake na mke wake yaliendelea kuwa mazuri au la.