Cheka Kidogo: Jamaa Ashusha Maombi ya Kufunga Ibada Wakati Ndio Kwaaza Inaanza..!!!


Kulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri tu pale Dar es salaam. Walikuwa wakisali kanisa moja la kilokole.  Mwanaume alikuwa na tabia ya kulala usingizi kila akiingia ibadani.


 Siku moja mke wake akagundua dawa ya kumfanya jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala kanisani. Unajua ni dawa gani hiyo?

Kukiwa tu ndo ibada imeanza, jamaa alianza kuuchapa usingizi na mke bila kukawia akamminya kwa haraka akamwambia,

Mke: “Mchungaji amekuteua ufunge ibada kwa maombi”
Mwanaume akasimama haraka na kuanza kushusha maombi makali ya kufunga ibada

Mume:“Baba katika jina la Yesu tunakushukuru kwa ibada nzuri, Asante kwa ujumbe wa leo kutoka kwa mtumishi wako Mchungaji, Asante kwa miujiza ya uponyaji. Tunaomba ututangulie tunapokwenda majumbani kwetu kupumzika, Kanisa  woote tuseme Amen”

HAKUNA ALIYESEMA AMEN badala yake baada ya kumaliza sala tu, alilishuhudia kanisa nzima likimkodolea macho huku wengine wakicheka sana, na wengine wakiwa midomo wazi na wengine wakiinama kwa aibu kwani ibada ndo tu ilikuwa imeanza na jamaa anashusha sala ya kufunga ibada!

Nimesikia kuwa huyo bwana aliacha hiyo tabia ya kulala lakini sikujua mahusiano yake na mke wake yaliendelea kuwa mazuri au la.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad