Aliyekuwa staa mkubwa wa muziki
wa Taarab Bongo, Mzee Yusuf ambaye kwa sasa amemrudia Mungu wake na kuwa
alhaji, amefunguka kuwa bado watu hawaamini kama kweli ameachana na
muziki wa kidunia hivyo wamekuwa wakimwalika kwenye misikiti mbalimbali
ndani ya Dar na mikoani hivyo kuwa mhadhiri wa kitaifa (kwa mujibu wa
Kamusi Sanifu, mhadhiri ni mtu anayetoa mhadhara, au mwalimu katika chuo
cha elimu ya juu hususan chuo kikuu).
Akizungumza baada
ya kuulizwa juu ya taarifa kwamba anafanya ziara kwenye misikiti
mbalimbali na kutoa mawaidha (kufanya mihadhara) ya kumtangaza Mungu kwa
nguvu zote, Mzee Yusuf alifunguka kuwa siyo kweli kwamba amepanga ziara
ya misikitini bali huwa anaalikwa kwa ajili ya kutoa mawaidha ya
Kiislamu.
“Siyo kwamba nimepanga ziara bali kila
ninapoingia kwenye misikiti mbalimbali kuswali, watu wamekuwa wakinitaka
nitoe neno kwa waumini hivyo nasimama, natoa mawaidha maana ndiyo
upande niliochagua kwa sasa wa kumtumikia Mungu wangu.
“Nimekuwa nikipata mialiko kutoka kwa
mashehe mbalimbali wa mikoani, ninakwenda kutoa neno maana watu wengi
hawaamini kama kweli nimeachana na muziki hivyo ninasafiri sana na
nikifika huko ndiyo wengine wanaamini na kuthibitisha.
“Kwa sasa nimeamua kusoma dini kiundani
ili nijue nini Mungu anataka na nini hataki, siyo kusoma Quran bali
nasoma dini niijue vizuri ,” alisema Mzee Yusuf, hata hivyo, watu
mbalimbali wanasema familia yake iko mguu sawa kujiandaa kufuata nyayo
zake.
Mwaka jana, Mzee Yusuf alitangaza
kuachana na muziki wa taarab kisha akaenda kuhiji Macca, jambo liliibua
mshtuko wa mashabiki wake lukuki wa bendi yake ya Jahazi.
Kwa Lugha nyingine tunaweza sema Mzee yusufu ameokoka, tena sio kuokaa kwa maneno au mdomo bali kwa vitende, matendo yake yanaonekana kweli ameamua kumfwata na kumtafuta muhumba na kuachana nayo yote ya kidunia Inshaallah Mwenyezi Mungu akusaidie akuongoze.
ReplyDeleteYesu ndiye njia, kweli na uzima, mtu haji kwa baba ila kwa njia ya Yesu. Mpokee Yesu ndio utafanyika mwana wa Mungu na utaurithi ufalme wa Mungu. Njia aliyoichagua Mungu ni moja tu, kumwamini Yesu ili umuone yeye Mungu. Amina
ReplyDeleteWewee usiwakwaze wenzio. Kila mtu na imani yake. Wewe una imani yako na mwenzako ANA imani yake, usionyeshe kujua kwamba uko sahihi, Kila imani Ina maneno yake ya kuvutia binadam ili awe. Karibu na muumba. Sasa sio pahali pale Hapa pa kuanza oooohoo huku hivi huku hivi. Please give people bleack with all mind set
DeleteNa wake zako pamoja na dada zako pia uwalinganie. Inshallah Allah akupe wepesi
ReplyDelete