Harmorapa na Wolper Feki. |
Msanii
chipukizi wa Bongo Fleva anayefanana sana kwa sura na msanii kutoka
WCB, Harmonize kiasi cha kubatizwa jina la ‘Pacha wa Harmonize’,
Harmorapa, leo ametinga kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-
Mwenge jijini Dar ambapo mbali na mambo mengine, amefungukia uhusiano
wake wa kimapenzi na ‘Wolper’.
Harmorapa amesema kuwa kutokana na
kufanana sana na Harmonize, aliamua kutafuta msichana anayefanana sana
na mpenzi wa Harmonize, mwanadada Jacqueline Wolper ambaye naye kwa
jinsi anavyofanana naye, ukikutana nao unaweza kudhani umekutana na
Harmonize na Wolper ‘orijino’.
Harmorapa
“Prodyuza wangu, Khalfan ndiye
aliyenikutanisha na mwanadada huyu ambaye watu wanamuita Wolper kutokana
na jinsi alivyofanana naye, alinikutanisha kwa lengo la kufanya naye
kazi akiwa kama video queen, akatokea kuwa rafiki yangu sana na mara kwa
mara nakuwa naye sehemu mbalimbali.
“Kiukweli uhusiano wetu ni wa kikazi tu tofauti na Harmonize na Wolper ambao ni wapenzi kweli.”