Jumapili mchana, picha za kijana
mmoja aliyetambulishwa kama Fredrick Richard zilianza kusambaa
mitandaoni, ikidaiwa kuwa amejinyonga, kisa ni mapenzi kwa mwanamke
mmoja ambaye alitajwa kwa jina la Rose, kabla ya baadaye jina hilo
kurekebishwa na kuwa Mariam.
Tukio hilo lililozua gumzo kubwa
lilidaiwa kutokea huko Korogwe mkoani Tanga, ikidaiwa kuwa marehemu
alichukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa mpenzi wake wa kike, ambaye
anadaiwa kuitwa Mariam, aliamua kumuacha na kuolewa na mwanaume
mwingine, ambaye alitajwa kuwa anaitwa Robert.Robert.
Katika ujumbe uliodaiwa kuandikwa na
marehemu huyo, alidai kuwa amechukua uamuzi wa kujitoa roho kufuatia
mpenzi wake huyo kumuacha yeye na kukubali kuolewa na mtu aliyetajwa
kuwa ni Robert, licha ya kuwa alipata huduma nyingi za thamani kutoka
kwa marehemu.
Aidha, ujumbe huo ulimtaja Robert kuwa
siyo tu ni rafiki wa marehemu, bali ni bosi wake, hivyo aliamua kutumia
cheo chake kama fimbo ya kumchapia. Sambamba na madai hayo, kulikuwepo
na picha zilizotajwa kuwa ndizo za mwanamke anayedaiwa kumkoroga
Fredrick, akionekana mrembo hasa, pia za Robert.
Kama ilivyo ada yake, RISASI MCHANGANYIKO liliamua
kuchimba ili kubaini ukweli wa tukio hilo ambalo licha ya kuzua maneno
mengi miongoni mwa wachangiaji mitandaoni, pia liliacha simanzi kwa
ndugu na jamaa wa wahusika hao.KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Benedict Wakulyamba alipatikana kupitia simu yake ya mkononi na baada ya
kuulizwa kuhusu tukio hilo, alikiri kutokea wilayani Korogwe.
“Taarifa hizo zimenifikia, tukio
hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita, katika mtaa wa Mbezi
wilayani Korogwe. Katika chumba chake alichojinyongea, marehemu aliacha
ujumbe mfupi uliosomeka;
“Asilaumiwe mtu yeyote, nimeamua kujinyonga mwenyewe kutokana na matendo yangu.”
Hata hivyo sisi tunaendelea kumtafuta mtu aliyeshirikiana naye kufanya hayo matendo kwa sababu hawezi kufanya peke yake,” alisema.
Mariam.
KUHUSU PICHA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI?
Alipoulizwa kuhusu kama marehemu ndiye
ambaye picha yake ipo katika mitandao ya kijamii, alisema amesikia juu
ya jambo hilo, lakini hawezi kuthibitisha kama huyo ndiye aliyejinyonga
na kuongeza kuwa polisi hawafahamu chanzo cha tukio hilo.
Chanzo chetu cha kuaminika kililidokeza
Risasi Mchanganyiko kuwa mtu anayeitwa Robert yupo na ni kweli ndiye
aliyeonekana katika picha akiwa kwenye gari, lakini hahusiani na habari
hizo hata kidogo. Chanzo hicho kilitoa namba za simu za kaka wa jamaa
huyo aliyefahamika kwa jina la Sheck, ambapo alipopatikana, alifunguka
hivi;
“Sisi tuna nyumba kule Korogwe, ambako
kaka yake Fredrick (marehemu) alikuwa amepanga. Ninamfahamu huyo kijana
kwa sababu alikuwa akija pale mara kwa mara, Robert anayetajwa siyo huyo
ambaye picha zake zipo mtandaoni, huyu ni mdogo wangu na haishi
Korogwe, yupo hapa Dar na ana mke na familia yake.
“Mara ya mwisho Robert kufika hapa
ilikuwa ni Krismas iliyopita na hata huyo Mariam mwenyewe hamfahamu,
kilichotokea naona watu wanataka tu kumchafua mdogo wangu kwa
kufananisha majina.”
Fredrick, akiwa amembeba mpenzi wake na Mariam, enzi za uhai wake.
UTATA JINA LA MARIAM
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya uhakika
wilayani Korogwe, ni kweli kwamba marehemu Fredrick alikuwa akishiriki
mapenzi na msichana mwenye jina la Mariam, lakini pia jina hilo ni la
dada yake. Baadhi ya majirani wanasema walikuta ujumbe unaodaiwa
kuandikwa na Fredrick ukitaka Mariam asihusishwe na kifo chake kwa namna
yoyote, hali inayowatia shaka ni yupi aliyelengwa, iwapo ni dada au
mpenziwe.
“Sasa inakuwa vigumu kuelewa ni Mariam
yupi ambaye anahusika na tukio hili ambaye marehemu alisema asihusishwe.
Kama ni dada yake pengine anaufahamu ukweli juu ya kilichotokea, lakini
hata kama ni aliyekuwa mpenzi wake, pia hakuna anayejua lolote, kama
amechangia katika kifo hicho au la,” kilisema chanzo hicho na kuongeza
kuwa mpenzi wa marehemu huyo, ambaye alikuwa akimiliki saluni wilayani
hapo ametoweka tokea kutokea kwa tukio hilo.
HUYU HAPA ROBERT, MSOME ANAVYOSEMA
RISASI MCHANGANYIKO liliweza
kumfikia Robert ambaye alikiri kuwa hilo ni jina lake na ndiye mwenye
picha zinazosambaa mtandaoni, lakini hana uhusiano wowote na tuhuma
zinazotolewa, kwani hata mwanamke anayezungumzwa hamfahamu na hata
alipoomba picha zake zaidi na kutumiwa, alishindwa kumtambua.
“Mimi siishi Korogwe na wakati tukio la
Fredy linatokea mimi nilikuwa njiani kurudi kutoka Kigoma kuja Dar
kikazi. Nimedhalilishwa, nimefedheheshwa sana, nimetukanwa, familia
yangu imezodolewa, mke wangu kila anapopita ananyooshewa vidole kuwa
mumewe nimesababisha kifo cha rafiki yangu.
“Nimesikitika sana na taarifa za uongo
zinazoenezwa mitandaoni ila nashukuru ndugu zake marehemu wamenipigia na
kunipa pole na kusema kuwa ukweli wao wanaujua kuwa si mimi ambaye
nahusika katika tukio hilo.”
MSIKIE MARIAM, DADA WA MAREHEMU
RISASI MCHANGANYIKO lilimpata
dada wa marehemu, Mariam ambaye alisema Robert asihusishwe na kifo
hicho kwani hakuna ukweli wowote. Wala huyo Robert anayetajwa kuwa
alikuwa na cheo kikubwa kumzidi kaka yake pia siyo kweli, kwani hakuwa
akifanya kazi zaidi ya kuwa mtu wa mishemishe tu za kawaida.
“Mimi ninachoona ni kuwa mdogo wangu
ameuawa. Kuna watu watakuwa wamemuua na ili kuficha ushahidi, ndiyo
wakamtundika na kuanza kueneza maneno ya uongo mitandaoni.”
FREDRICK NI NANI?
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Fredrick
alikuwa ni ofisa mikopo katika Saccos iliyomilikiwa na familia yao,
iitwayo Single Microfinance Company akiwa amezaliwa mwaka 1989 na
alizikwa Jumatatu katika Kijiji cha Kongoto, kilichopo Butiama mkoani
Mara.
MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA
“Ni kweli tukio hilo limetokea ila
habari zinazoandikwa kwenye mitandao ya kijamii nyingi zinaongezewa,
zinapotosha ukweli, barua inayosambazwa kuwa imeandikwa na marehemu na
ile inayodaiwa kuandikwa na Mariam siyo zenyewe, marehemu aliacha
kipande kidogo cha karatasi, sijaona mtu ambaye ameshikiliwa na polisi
kuhusu tukio hilo ila nadhani wanaendelea na uchunguzi wao,” alisema
mwenyekiti huyo, Rajabu Nzige.
Mwisho
Ninachoona ni kuwa huyo mpenzi wa marehemu hataki kuchafuliwa hataki watu wamuelewe vibaya kuwa amesababisha kifo cha marehemu ndiyo maana anajisafisha ili watu wasimchukie, ukweli ni hivi huyo demu wa marehemu ameolewa na bosi wa marehemu na ndiyo maana marehemu kajinyonga, sababu huyo bosi ana mihela ndiyo anajaribu kujisafisha ili watu wasimuelewe vibaya na ndiyo maana habari yenyewe haieleweki, mara mariam ni dada wa mpenzi wa marehemu yaani haileweki sababu ya uwongo na marehemu hajauliwa na mtu bali amejinyonga na mtu wa kumlaumu ni mpenzi Wake ambaye ameolewa na bosi wa marehemu, huo ndio ukweli
ReplyDelete