FEROOZ " Inaniwia Vigumu Kuacha Madawa ya Kulevya"

Msanii mkongwe wa muziki Ferooz Mrisho ambaye katika miaka ya 2000 alitamba na wimbo wa Starehe ambaye kwa sasa ameathirika na dawa na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai inamuwia vigumu kuachana na matumizi ya dawa hizo. Muimbaji huyo amedai amejikuta akitenga bajeti kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia dawa.

“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie dawa maana ni vigumu kuacha. Natamani sana kurudi kama zamani ili heshima yangu iwepo ila inanisumbua, lakini naamini iko siku,” Ferooz aliliambia gazeti la Mtanzania. Hata hivyo muimbaji huyo alipoulizwa ni wapi anaponunua Madawa hayo hakuwa tayari kutaja.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu ndiye wa kuanza nae, halafu wengine wafuate, me naona kama suala lamadawa ya kulevya watu hatujalipa uzito stahiki. Hii vita haitaji kuona huruma hawa watumiaji watuonyeshe hizi dawa wanapata kutoka kwa nani halafu atataja hadi kule zinapotoka kuingia nchini mwetu.

    ReplyDelete
  2. Hivi nyie mnawajua wanaokula unga au hamuwajui? awataje wauzaji halafu akitaka kununua ataenda kwa nani, mateja sio wanywa pombe, mnacheza na mateja ama nini, teja hata ukimchapa haachi unga, kwanza teja akiacha kula unga ataumwa sana na ndiyo maana wengi wanaogopa kuacha sababu wanaogopa kuumwa, mtu ukiacha pombe sana sana utapata hang over kesho yake baada ya hapo mtu unasikia fresh kama kawaida lakini sio unga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad