Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ametembelea shamba lake la kilimo cha kisasa cha mboga mboga (Green House) yaliyopo Hain na kuwajulia hali wafanyakazi pamoja na wataalam wake leo Ijumaa.
Pia, Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa nayo ya kupoteza ajira zao wanazozitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasiu Byakanwa kupiga marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe.
Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani shamba hilo lipo ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.
Kwa madini yenye kuchafua vyanzo vya maji yanayomilikiwa na wageni hayafungwi. Namtumbo mnataka kuvua Uranium ambayo ni sumu zaidi na itaathiri mito na maji ya kunywa bado mnatarajia kufanya hivyo. Je ipi ni hatari zaidi. Na waathiriwa wangapi. Tanzania ebu tukae chini na kujitafakari upya, Tumeuingiza ukoloni mamboleo unaharibu mazingira, na tunatoa rusa kuua wanyama pori kwa wageni, madini yanayochimbwa kwa wingi na watu kuumia. Je elimu yetu ni ya chini au vipi. Je tumetawaliwa kimawazo au je. Je sisi tunainferiority complex kwa wazungu mpaka leo na kuamua kunyanyasana wenyewe kwa wenyewe. Ndo huu uhuru, Je ndo haya maendeleo ya Wanachi. Inaonekana Watanzania wengi wanashangilia. Kitu kikubwa fikra ndogo, uvivu kufikiri, Elmu duni. Taifa linarudi nyuma kama watu wengi hawajui au hawana uhuru na uwezo wa kufikiri. Ni hatari kubwa kwa kizazi kijacho .
ReplyDeleteSawasawa mdau wa hapo juu na comment yako wabongo wanajiona wamepanchi kumbe hawajui wamelikalia kaa la moto na kujumlisha elimu duni na dhaifu ipatikanayo bongo basi wengi hawana uwezo wa kuiona kesho itakuwaje kwenye visions zao
ReplyDelete