Mkuu wa Gereza la Kilimo Songwe, Lyzeck Mwaseba ameiomba Serikali kulipatia wafungwa wengi na pembejeo ili kuongeza uzalishaji.
Miongoni mwa pembejeo hizo ni majembe, matrekta na mitambo mingine ya kilimo.
Mwaseba aliwasilisha ombi hilo mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea gereza hilo ikiambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni.Ziara hiyo ililenga kujionea uzalishaji wa mahindi unaofanya na wafungwa.
“Gereza hili lina ukubwa wa hekta 2,170, lakini hivi sasa zinalimwa eka 250 kutokana na kuwapo wafungwa 165 tu ambao ni wachache,’’ alisema.
Tafadhalini wana magereza na wizara ya mambo ya ndani. hamisheni wa ukonga na arusha na isanga wanaotumikia kifungo waende kuzalisha huko. Fikira na Ombi ni zuri na ni tekelezi. Hapa kazi tu hakuna kula bure katika magereza yetu. Na kina goless wote wapelekwe huko kuzalisha....
ReplyDeleteSasa tumefikia huko?Balaa duniani
ReplyDelete