Gigy Money amshika uchawi Amber Lulu

 VIDEO Queen matata Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameanza mwaka mpya kwa kushusha madai makali kuwa Video Queen mwenzake Lulu Euggen ‘Amber Lulu’, anamroga na anaishi kwa kutumia nyota yake.

Akizungumza na gazeti hili Gigy alisema kuwa kuna vitu vingi sana amekuwa akifanyiwa na mrembo huyo kitu ambacho alikivumilia muda mrefu hivyo kwa sasa ameona ni bora kuviweka wazi.


“Unajua Lulu, mimi nilikuwa nampenda sana kama ndugu yangu kabisa lakini naona vitu vyangu vingi haviko sawa ukifuatilia kwa wataalam unaambiwa ni yeye (Amber),” alisema Gigy.

Alipoulizwa Amber kuhusu tuhuma hizo, alisema: “Sijamroga yule, ana kipi? Aseme tu nimemzidi maarifa na kujitambua.”

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Gigy Money kama unamuamini Mungu mtu yeyote hawezi kukuroga, umrudie Mungu hayo yote yataisha, hata uchawi hauna nguvu kama za Mungu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad