“Gigy Money Hawezi Kuwa na Rafiki Kama Mimi, Atajivunia Sana” – Amber Lulu

‘Video qeen’ kutoka Bongo ambaye naye amejitosa kwenye uimbaji wa Bongo Fleva, Amber Lulu amemshambulia mwenza ambaye pia ni video qeen, Gigy Money, na kusema hata siku moja hawezi kuwa na urafiki na mtu kama huyo.

Amber ametoa mashushu hayo kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio ambapo amesema licha ya kufanya kazi zinazofanana, hawezi kuwa na ushkaji naye na ikitokea hivo atajivunia sana.

“Gigy Money hawezi kuwa na mwana kama mimi, atajivunia sana, hawezi kuwa mshkaji wangu, sina mahusiano naye wala sina beef naye, hawezi kuwa kwenye cycle yangu”

Msikilize mwenye hapa akifanya mahojiano na Jay R Junior.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi namuona gigy money ni msheshi sana na pia anajelewa sana na anochokifanya ingawa ana umri mdogo na pia ni mrembo sana na analo umbo zuri sana kuuliko amba lulu hapo amber lulu anamuonea donge gigy money

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad