Utafiti
uliofanywa na shirika la Oxfam la Uingereza unaonesha mabilionea wanane
wanamiliki mali sawa na mali ya watu 3.6 bilioni kwa pamoja.
Takwimu za shirika hilo, ambazo
zimepingwa na baadhi ya wakosoaji, zinatokana na maelezo na habari za
kina zilizokusanywa na shirika hilo, na zinaonesha pengo kati ya
matajiri na maskini ni kubwa kuliko ilivyodhaniwa awali.
Ripoti hiyo ya Oxfam imetolewa wakati
mkutano mkubwa kuhusu uchumi wa dunia unaanza mjini Davos. Mark
Littlewood, wa Taasisi ya Masuala ya Uchumi, amesema Oxfam badala yake
wanafaa kuangazia njia ya kusisimua ukuaji.
“Kama shirika linalopiga vita umaskini, Oxfam wanaonekana sana kuangazia zaidi matajiri,” Mkurugenzi mkuu huyo wa shirika hilo la ushauri amesema.
Kwa wale ambao wana malengo ya “kutokomeza kabisa umaskini uliokithiri”, sana wanafaa kuangazia hatua za kusisimua ukuaji wa uchumi, ameongeza.
Ben Southwood, ambaye ni mkuu wa utafiri
katika Taasisi ya Adam Smith, amesema la muhimu zaidi si kiasi cha mali
inayomilikiwa na watu matajiri zaidi duniani, bali ni hali ya maisha ya
watu maskini zaidi duniani, ambayo inaimarika mwaka baada ya mwaka.
“Kila mwaka, tunapotoshwa na takwimu
za Oxfam. Takwimu ziko sawa – zinatoka kwa Credit Suisse – lakini
ufasiri wa takwimu hizo si sahihi.”
‘Mkutano wa Davos‘
Mkutano unaofanyika mjini Davis, Uswizi huwavutia viongozi wengi wa kisias ana kibiashara duniani.
Katy Wright, mkuu wa mambo ya nje wa
Oxfam, anasema ripoti hiyo imesaidia shirika hilo kuwauliza maswali
viongozi wa kisiasa na kiuchumi.
“Tuna uhakika kwamba Davos ni
mkutano tu mwingine wa kupiga gumzo miongoni mwa viongozi na watu wenye
ushawishi duniani, lakini tunahitaji kujaribu na kupata mwelekeo,” aliongeza.