Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 32
kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Vitu Laini linalofanya safari zake
kutoka vijiji vya Kilolo kwenda Iringa Mjini kugongana na lori la mbao
karibu likiwa limekaribia kufika Iringa Mjini.
Akizungumza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Peter Kakamba amethibitisha
kutokea kwa ajli hiyo na kueleza kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo
wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.“Ni
kweli ajali imetokea leo asubuhi nje kigogo ya Mji wa Iringa, basi
ndilo limelogonga lori kwa nyuma na kusababisha kifo cha mtu mmoja
aliyeaga dunia palepale na kusababisha majeruhi 32.
“Majeruhi wote tumewapeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa ambako wanaendelea kupatiwa matibabu mpaka sasa. Alisema Kamanda Kakamba.Kuhusu
chanzo cha ajali hiyo haijafahamika kama ni matatizo ya gari au
mwendoksasi wa dereva hivyo Kamanda Kakamba amesema watatoa taarifa
rasmi baabdaye kuhusu tukio hilo.
Basi lenyewe limechoka ile mbaya, kweli serikali inaruhusu mabasi kama haya yabebe abiria kweli? Ndiyo maana kila kukicha ajali haziishi, kule dar kuna mabasi mapya ya mwendo kasi, kwa nini mabasi mapya yasitolewe nchi nzima ili kuepuka ajali kama hizi na kuwaokoa watu, sababu watanzania watakwisha na ajali kama hizi zimeua wananchi wengi sana sababu sasa hivi watu wengi wanakufa na ajali kuliko magonjwa
ReplyDelete