Mwalimu mmoja wa Shule ya elimu ya kati ya Houston, Marekani, Alexandria Vera (24).
Mwalimu mmoja wa Shule ya elimu ya kati ya Houston, Marekani,
Alexandria Vera (24) amehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya
kukutwa na hatia ya kutoka kimapenzi na mwanafunzi wake hali
iliyopelekea mwalimu huyo kupata mimba.
Akitoa hukumu kwa mwalimu huyo, Hakimu wa Mahakama ya Houston,
Michael McSpadden alisema hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa walimu
wengine kwani wanataka walimu wawafundishe wanafunzi na sio kufanya
mambo mengine.
“Tunataka wanaotoa elimu wawafundishe wanafunzi wetu, tunahitaji mikono yao iwe mbali na wanafunzi,” alisema McSpadden.
Aidha McSpadden alisema alitaa kumpa adhabu ya miaka 30 gerezani
lakini aliamua kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa na mimba ya
mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akimfundisha shuleni na kuishi nyuumba
moja.
Awali Alexandria Vera alisema kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na
mwanafunzi huyo mwaka 2015 wakati alipokuwa darasa la nane na baada ya
hapo walianza kuishi pamoja lakini kwa ruhusa ya wazazi wa mwanafunzi.
Alisema wazazi wa mwanafunzi huyo walikubali wawili hao kuishi nyumba
moja ili awe anamfundisha lakini walianza kuwa wakishiriki tendo la
ndoa karibu kila siku jambo lililosababisha mwalimu kupata mimba.
Nae mmoja wa wanafunzi wa shule ambayo mwalimu huyo alikuwa
akifundisha alisema kuwa amewahi kushuhudia mwanafunzi
mwenzake akimshika mwalimu makalio mbele ya darasa bila mwalimu kuchukua
hatua yoyote.
Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa