MAREKANI: Mfanyibiashara mmoja nchini Marekani ambaye amezozana na
idara ya magari nchini humo DMV amelipa kodi yake ya dola 3,000 kwa
kutumia mikokoteni mitano iliojaa sarafu 300,000.
Nick Stafford kutoka Cedar Buff,
Virginia, aliwasilisha sarafu nyingi hatua iliolazimu mashine ya
kuhesabu sarafu hiyo ya Idara hiyo kushindwa kuzihesabu. Hatua hiyo
imekuja kufuatia mgogoro kati yake kuhusu kuwasiliana na wafanyakazi wa
mamlaka ya mapato nchini humo kuwauliza kuhusu kodi yao.
Iliwalazimu wafanyakazi kutumia saa saba
wakihesabu sarafu hizo hadi usiku. Walimaliza kazi hiyo ya kuhesabu
mapema siku ya Alhamisi.
Bwana
Stafford aliwasilisha pingamizi yake kwa sababu alizitaka idara za
serikali kuangazia na kutoa majibu kwa maswala yanayowakumba raia.
“Haijalishi iwapo utalipa dola 300
kwa mwaka kama kodi au dola 3000 kwa mwaka kama mimi kwa sababu uti wa
mgongo wa taifa lililo na demokraisa huru ni sharti liwe na serikali
ilio na uwazi,” alisema.
Bwana Stafford ameelezea katika mtandao
wake kwamba mgogoro wake na DMV ulizuka kwa sababu idara hiyo haikutaka
kumpatia nambari za simu za moja kwa moja kuhusu afisa wa kuwasiliana
naye ili kusajili magari matatu na kulipa ushuru kwa kuwa anamiliki
nyumba tatu katika maeneo 3 tofauti.
Aliwasilisha
ombi la kutaka kupewa nambari ya moja kwa moja kulingana na Bristol
Herald Courier na akapewa nambari ya simu ambayo angepiga. Lakini
alipoitumia aliambiwa kwamba haingeweza kuitumia kuuliza maswali.
Bwana Stafford alitaka kujua nambari
hizo za moja kwa moja za maafisa wengine tisa ijapokuwa Idara hiyo
tayari ilikuwa imemshughulikia swala lake. Na ombi lake lilipokataliwa
alienda mahakamani kuwasilisha malalamikoi yake.
Mapema wiki hii jaji mmoja alipinga
maombi yake matatu aliowasilisha, akikataa maombi alilowasilisha kwa DMV
na wafanyikazi wake wapigwe faini.
Hata hivyo wafanyikazi wa idara ya magari baadaye walimpatia nambari hizo alizotaka na tayari amezichapisha katika mtandao wake.
Bwana Stafford anasema kuwa idara ya
magari ililazimika kukubali malipo yake kwa sababu sheria ya Marekani
kuhusu sarafu mwaka 1965 inasema sarafu ni fedha halali na zinaweza
kutumika kulipa madeni, kodi na mishahara