Rais wa awamu ya nne wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amepata
nafasi ya kukutana na mabilionea wawili wakubwa duniani akiwa ziarani
Davos nchini Uswisi.
Rais Jakaya Kikwete alikutana na tajiria namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote kutoka nchini Nigeria na tajiria namba moja duniani, Bill Gates kutoka nchini Marekani.
Viongozi hao wamekutana nchini Uswisi katika Mkutano wa Dunia wa Uchumi (World Economic Forum) wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo wa uchumi wa dunia.
Mbali na masuala ya uchumi, mkutano au kongamano hilo pia hujadili kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa sasa yamekuwa ni tishio kubwa kwa viumbe mbalimbali.
Mkutano huu huudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali pamoja na asasi nyingine za kuraia zikiwa na lengo la kuweka nguvu pamoja na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.