Inasikitisha Mnoo..Soma Hapa Alichokisimulia Mmoja ya Waliofukiwa na Kifusi Mgodini Jinsi Walivyokuwa Wanaishi Chini ya Ardhi Kwa siku Tano..!!!


Uji, biskuti na maji waliyotushushia jana ndivyo vilivyorudisha uhai wetu,” hayo ni maneno ya mmoja kati ya wachimbaji 15 waliookolewa katika mgodi wa RZ walikokuwa wamefukiwa na kifusi kwa siku tano.

Mchimbaji huyo, Mgalula Kayanda alisema hali yao ilikuwa mbaya na mwenzao mmoja alishakata kauli lakini maji yaliwafanya wawe na nguvu.

Na niliamini hata nisipotoka leo, sitakufa tena,” alisema baada ya wote kuokolewa jana.

Kayanda alisema waliingia mgodini saa nne usiku na kuanza shughuli za uchimbaji na saa nane usiku walisikia kishindo kikubwa huku wenzao wakiwaita watoke nje.

“Tukiwa chini tulisikia tukiitwa na waliokuwa nje, wakitueleza tusogee kunatitia, baada ya kusikia wote tukakaa sehemu moja na ghafla umeme ukakata, kukawa giza, hakuna mawasiliano na hewa ikawa haingii,” alisema.

Huku wakiwa hawajui majira kutokana na giza, mpira mmoja wa kupitisha hewa ulianza kufanya kazi na kuwapa tumaini, lakini changamoto kubwa ilikuwa njaa.

Mwenzake Jackson Lucas,  mwenyeji wa Tabora alisema walikua umbali wa mita 100 chini ya ardhi lakini walipopata taarifa kutoka kwa wenzao kuwa ardhi inatitia, walipanda na kukaa sehemu moja kusubiri muujiza wa Mungu.

Lucas alisema hali mbaya ya hewa iliyosababishwa na harufu ya kinyesi ilikuwa moja ya changamoto ya kukaa katika shimo hilo kwa siku nne.

Hata hivyo, juzi msemaji wa kampuni ya RZ, Francis Kiganga alisema shimo lililofukiwa na udongo lina urefu wa mita 38 kwenda chini na pembeni kuna njia yenye urefu wa mita nyingine 38.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakika Jina linalozidi Majina yote Litukuzwe.

    ReplyDelete
  2. Kweli Mungu anaishi. Wasisahau kumshukuru Mungu tuu!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad