Inasikitisha Sana:Auawa na Kutupwa Chini ya Daraja,Kisa Hiki Hapa..!!!!


MKAZI wa kijiji cha Sakalilo kilichopo mwambao wa Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Kalitus Jacob (44) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kisogoni kisha mwili wake ukatupwa chini ya daraja la Mumba na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema tukio hilo lilitokea Januari 16 mwaka huu, saa 12:00 jioni katika kijiji cha Sakalilo “Kabla ya tukio, alionekana akiwa kilabuni na wake zake wawili wakinywa pombe, aliwaaga na kuondoka na hakurudi tena hadi alipokutwa akiwa amekufa. Chanzo cha mauaji hakijajulikana na juhudi za Jeshi la Polisi zinaendelea ili kubaini kiini cha mauaji hayo,” alieleza Kamanda Kyando.

Alisema kuwa mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya maandalizi ya maziko yake baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

Alisema watuhumiwa hawajakamatwa huku uchunguzi unaendelea ili kuweza kuwabaini waliohusika katika mauaji hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad