Hatimaye Msajili wa
Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema anamtambua Profesa
Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif ni Katibu Mkuu.
Amesema hana hofu ya kuchafuliwa kutokana na tuhuma zinazotolewa dhidi yake.
Kauli
ya Jaji Mutungi imekuja baada ya taarifa na kauli za matusi na kejeli
zilizomuhusisha yeye na ofisi yake kusambaa kwenye mitandao mbalimbali
ya kijamii baada ya kuidhinisha zaidi ya Sh300 milioni za ruzuku kwenda
kwenye akaunti ambayo kamati ya uongozi ya CUF ilidai siyo ya chama
hicho.
Taarifa
za msajili kuingiza fedha hizo kwenye akaunti hiyo na baadaye kutolewa
kwa njia inayoonekana kutia shaka zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya
Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ambaye alilinganisha suala hilo na
uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta
Escrow.