Jengo la Ghorofa Tatu Lamporomokea Mtu Zanzibar..!!!


Jengo la ghorofa tatu lilokuwa katika ukarabati katika Mjimkongwe wa Zanzibar  limeporomoka na kuua mtu moja  na mwengine kujeruhiwa vibaya.

Jengo hilo la ghorofa tatu ambalo liko katika mtaa wa Mjimkongwe  lilianguka wakati mafundi wawili wakiwa wako kazini na ghafla ukuta wa mbele ukaporomoka na kuwatupa barabarani  ambapo moja ya fundi  huyo,  aliokolowa na wananchi na kumpeleka hospitali kuu ya Mnazimoja  huku hali yake ikiendelea kuwa nzuri ,lakni pamoja na jitihada za kikosi cha ziamamto na wananchi kujaribu kumuokoa fundi mwingine hazikufanikiwa na fundi huyo  alifariki baada ya kufukuliwa na kikosi hicho  na maiti yake kupelekwa hospitali kuu ya Mnazimoja  kwa uchunguzi kabla ya familia kukabidhiwa kwaajili ya maziko ambapo kamanda wa polisi Mjinimagharibi Kamishna Msaidizi mwanadamizi wa polisi Hassan Nasser alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Wakizumgumza   mashuhuda walioshudia jengo hilo likiporomoka  ambalo ni mali yawakfu na mali amana wamesema ilikuwa ni mshutko mkubwa  ambao uliwashtua wananchi wa hapo lakini bahati nzuri hapakuwepo na wapita njia wakati udongo na mawe yakiporomoka ingawa ni pikipiki moja iliyokuwa imeegemezwa ilifunikwa  huku injinia wa mamlaka ya Mjimkongwe  Mussa Awesu Bakari amesema ujenzi wa jengo hilo ulikuwa unafanyika kwa mujibu wa sheria na taratibu zote za mamlaka ya Mjimkongwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad