Jinsi Kijana wa Miaka 22 Alivyombaka Mtoto wa Miaka 5 Karibu na Ziwa Victoria..!!!


Kijana aliyejulikana kwa jina la Petro Magayane miaka 22 mkazi wa Igombe Jijini Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumbaka na kumjeruhi katika sehemu zake za siri mtoto mwenye umri wa miaka 5 ambaye ni mkazi wa eneo hilo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 23.01.2017 majira ya saa 2 usiku katika kijiji cha Igombe “A” kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa akiwa amelewa  alifika maeneo ya nyumbani anapoishi mtoto huyo kisha akamtuma dukani maeneo ya mwaloni Igombe.

Aidha baada ya muda mchache kupita mtuhumiwa alimfuata mtoto huko dukani kisha kumfanyia ukatili wa kumbaka na kusababisha majeraha na maumivu makali katika sehemu za siri za mtoto huyo.

Wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo, askari walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye yupo katika mahojiano na jeshi la polisi, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Msangi amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha tukio hili ni ulevi. Mtoto amepatiwa matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad