JINSI Mramba wa Tanesco Alivyotumbuliwa..Sababu Zatajwa


Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba.

Taarifa ya Ikulu ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa ilisema uamuzi huo ulichukuliwa na jana na papo hapo akamteua msomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Tito Esau kukaimu nafasi hiyo.

Uamuzi huo ambao haukueleza sababu, umechukuliwa muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwaweka kikaangoni vigogo waliotangaza kupandisha bei ya umeme, akisema hatua hiyo ni ushahidi kuwa bado kuna majipu na ataendelea kuyatumbua.

Juzi, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ilikubali maombi ya Tanesco ya kupandia bei ya umeme kuanzia Januari Mosi kwa asilimia 8.5, hatua ambayo ilizuiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo huku Rais Magufuli akisema hatua hiyo ilikuwa inakwamisha mipango ya Serikali inayojiandaa kuelekea katika uchumi wa viwanda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad