Jinsi Wanadunia Tunavyoandaliwa Kuwa Mazombi na Maroboti Bila Kujua..!!


Unaweza ukapaniki nitakapokwambia mawazo mengi unavyodhani ni yako sio yako ni vitu ulivyopandikiziwa Bila kujua. Sisi tunaamini uwepo wa Mungu na uumbaji tunaamini pia Mwanadamu aliumbwa na Uwezo huru wa kufikiri na kuchagua.

Vita kubwa inayoendelea Sasa chini ya ardhi sio dhidi ya Magaidi, waasi au religious extremists Bali ni kumuondolea mwanadamu zawadi hii ya pekee aliyopewa na Mungu na vita hivi hadi sasa imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 50 duniani kote. Waandisi jamii ndio Moyo na silaha ya maangamizi katika vita hivi.
[​IMG]
Lengo la bandiko hili sio kutishana Bali ni kuongeza uelewe halisi wa mambo maana ushahidi usio na Shaka umeonyesha kujua michezo hii kutakupunguzia asilimia kubwa ya kuwa muhanga wa janga hili. Mambo haya yanafanyika kupitia Mind control techniques,Brain Washing techniques, subliminal sensations na vifaa vikubwa vinavyowezesha ni TV, Movies, Adverts, Social Media hivi ndio mama.

Zifuatazo ni jinsi 06 unavyoweza kunaswa katika mtego ya kutawaliwa bongo

1:Matangazo ya Biashara na Propaganda
[​IMG]
Asilimia kubwa ya watu wanavyovaa, kula, kunywa, kunyoa style, aina ya vitu wanavyopenda sio matokeo ya uamuzi wao wa Hiyari Bali Matangazo na ushawishi wake.

 Leo duniani habari ikathibitika kama ni ya kweli, au kitu kitaonekana ni sahihi au kizuri au chafaa kutumika katika jamii kama kimeandikwa kwenye vyombo vya habari mbalimbali vya kimataifa visivyohusiana. Lakin ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya habari zinazoenea duniani na asilimia kubwa ya vyombo vya habari vikubwa ulimwenguni vinamilikiwa na Makampuni sita tu tena yenye uhusiano wa karibu.

 Kwa maana nyingine wanaweza kuamua kuja na habari yoyote kukuaminisha jambo lolote wakati wowote. Simaanishi tusiangalie habari Bali tujiongeze kwa akili zetu pia ktk kupambanua. Kwa nini kuna uwezekano zikwepo jumbe (subliminal messages) ambazo zimechujwa na kurushwa kwenye media zote duniani Bila kujua asilimia kubwa zinauhusiano au Kuna mipango nyuma ya propaganda hizo.

 Leo Kuna watu wanawachukia waarabu kwa sababu media zimesema, na Kuna watu wanawachukia wamarekani kwa sababu media zimesema wanawaonea waarabu.Mfano kwenda kuangalia Movies ukiwa na Bisi na Soda au wanawake kuacha vifua nusu wazi au kutamani kuwa na vifua/boobs vikubwa wengi sio kwa hiyari zao bali ni matokea ya group thinking inayotokea kidogo kidogo ila kwa uhakika.
2:Watu kupangwa kukubali matukio kabla hayajatokea /Predictive programming
Dhana hii bado wengi haiwaingii akilini. Hii mbinu inatumika kwa mapana na kwa Muda mrefu hasa kupitia werevu wa Hollywood, Kuna vitu vingi ambayo zamani vilionekana kama ni fiction lkn Sasa katika jamii vimekubalika. Mfano mdogo kwenye cartoons Mind Blowing Examples of Predictive Programming in Cartoons | The Ghost Diaries

3:Michezo, Dini na Siasa na Ushabiki wa Mipira ya kimataifa
[​IMG]
Vitu hivi navyo kwa sehemu Kubwa vimechukua sehemu ya fikra za mwanadamu huru. Tuliwaona wafuasi wa kibwetele wakiteketea kwa moto kanisani ili waende mbinguni kama matokeo ya kutawaliwa fikra na kuoshwa ubongo. Michezo ilipaswa kuwa sababu kubwa kuleta umoja na afya, leo imekuwa kichocheo cha uadui kama zilivyo siasa. Umoja wa msingi kwa mambo yenye manufaa umekufa kutokana na akili zinazokumbatia mipasuko ya kisiasa, michezo na dini. Ukiangalia duniani hakuna vita ambayo dini na siasa haitakuwepo hata kwa mbali.

4:Vya kila, Vinywaji na Hewa
[​IMG]
Tunaishi kwenye dunia ambayo Mtu akiishi chini ya hewa bandia ndio tunamsifia na kumuona anapewa na ndio wa kuigwa, vyakula vilivyojaa sumu, maji yaliyojaa contents ambazo zingine hazieleweki kwa nini siwepo na kwa kiwango hicho ndiyo vinavyosisitizwa kila kona hata penye uwezekano wa kupatikana vitu Asili na original. Vitu hivi vimethibitika kushusha Uwezo wa kiakili, vingine vinahamasisha hasira na jazba, vingine vinadhoofisha Uwezo wote wa mwanadamu taratibu ila kwa uhakika.

5: Madawa na addictions
[​IMG]
Lengo kuu la wenye hekima na werevu wachache duniani ni kuhakikisha kila mmoja anakuwa addicted na kitu kinachomshusha Uwezo wake, kama sio drugs, movies, football, video games, pornography, chochote kile. Silaha kubwa ni kuhamasishwa kwa uwepo wa gonjwa la akili au saikolojia na kuwafafaua au kuwaelezea watu wote duniani au kwenye taifa flani kwa mwelekeo wa ugonjwa wa akili badala ya mwelekeo wa Uwezo wa mwanadamu kiakili. Na madhara yake wengi wanajikuta wako katika misongo na kujishuku kama wako Sawa, na hii inatengeneza mwanya wa kuweka rehani Uwezo wake wa kibinadamu na kukabidhi wengine wampangie cha kufanya.

6:Computers, TV na Smartphone/simu [​IMG] [​IMG]
Vitu hivi vyote sio vibaya, ila kwa dunia ya Sasa vimetengeneza uteja kw kuweka visismuzi vitakavyokufanya usibanduke. Social engineers au waandisi jamii wanaweka vitu vitakavyokufanya usibanduke na kuwepo kwako mbele ya screen kwa muda mrefu Kuna effects hadi ndani ya ubongo.

 Melatonin ni hormone inayotawala mzunguko wa usingizi kwa mwanadamu. Adui namba moja wa hormone hii ni mwanga hasa pale unapohitaji usingizi. Kukaa mbele ya kioo muda mrefu hasa usiku kutaathiri mzunguko wako wa usingizi. 

Kumbuka pale tunapolala ndipo ubongo unapata muda wa kujifanya usafi na kujiweka Sawa, madhara ya kukaa na simu au mbele y TV muda mrefu hasa usikuni kutengeneza shambani la kujitoa muhanga dhidi ya ubongo wako.

Mwisho :mwanadamu ni kiumbe mwenye Uwezo mkubwa, kuweka rehani Uwezo huu na kutufanya kuwa watumwa wawanadamu wenzetu ni kitu cha kukiepuka na kukikwepa sana. Unaweza usiamini au ukaamini ila lengo hapa nikuongeza ufahamu wa mambo ili kuongeza uelewe zaidi wa mienendo yetu.

Nini kifanyike

njia kuu ni kuwekeza zaidi ktk kusoma vitabu vinavyofikirisha na kukufanya utoe maoni yako kabla upinge au uunge mkono. Movies, TV programs nyingi, news nyingi zimekutwa programmed
Ukusisimua na sio kuufikirisha. Vipindi na scripts nyingi zinapelekwa haraka haraka ili ukoswe muda wa kufikiri.

Kama unaamini bibilia chukua Muda jisomee pia inashuriwa ujiunge na vikundi au taasisi za kidini zinzazotoa kipaumbele mijadala yenye changamoto na sio kuburuzwa na kuambiwa cha kufanya muda wote. Jifunze jinsi ubongo unavyofanya kazi hasa sehemu hisa Conscious na Subconscious Minds.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad