Kalapina Amlaumu Mama Chid Benz Kwa Kumdekeza na Kumwendekeza Chid Benz Mpaka Ameshindwa Kuacha Madawa

Rapa Kalapina ambaye ni mwanaharakati wa kuwasaidia watu ambao wameingia kwenye matumzi ya dawa za kulevya amefunguka na kusema kuwa mama yake mzazi Chid Benz kama mtu anayemuendekeza Chid na kumfanya asitoke kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Kalapina amesema mama huyo anampenda sana mtoto wake kiasi cha mtoto kujua na kuona kwamba hata akifanya jambo fulani yupo mama yake ambaye atasimama na yeye.

Kalapina alisema hayo jana kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusema wazazi wengi wamekuwa chanzo cha watoto wao kuingia kwenye matumzi ya dawa za kulevya na kuingia hata kwenye mahusiano ya jinsi moja sababu ya wazazi wamekuwa wakiwadekeza sana watoto au kuwapa uhuru mkubwa na kuruhusu maisha ya uzungu kutawala.

"Kiukweli mama yake mzazi Chid Benz anampenda sana mwanaye na hali hiyo inampelekea mdogo wangu yule kuona hata nikizingua mama atanitafuta tu, au kuona mama atasimama na yeye tu sababu mama yake anampenda sana, lakini siyo Chid Benz tu wazazi wengi wanawalea watoto kwa kuwadekeza sana, wazazi hawana muda na watoto na hili linachangia vijana kuingia kwenye madawa ya kulevya hata kwenye ushoga pia, lakini sisi wazazi wetu zamani ulikuwa ukizingua unapigwa sana hivyo lazima utanyooka tu" alisema Kalapina.

Source:EATV
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kaka Kalapina usiseme hivyo sote tuwaombee watoto wetu kuwatowa kwenye janga hilo najuwa kuna watu wazima wana watoto sitili wanaingia kwenye haya majanga.

    ReplyDelete
  2. Mimi nimeanza kuishi peke yangu nikiwa na miaka 19 na sina mawasiliano na wazazi na wala sitokuja kuongea nao kwa hiyo nipo huru lakini sijawahi kutumia madawa na wala sitowahi kutumia chid benz ni mtu mzima hata kama akidekezwa na wazazi lakini uwamuzi ni wake kama akiamua kuacha madawakuna wazazi wanawapenda watoto wao hata kama wakiwa machangu doa na wazazi kuwapiga watoto haisaidii kitu mimi mwenyewe nimepigwa sana na wazazi kunifanya niwe jeuri leo hii sitaki kuongea na wazazi wangu na simuamini mtu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad