Kamanda Mpinga Akanusha Trafiki Kulipwa Bonasi Kwa Kukamata Magari

Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imesema hakuna polisi yeyote wa kikosi hicho anayelipwa bonasi kutokana na ukamataji na ulipaji wa faini zinazotokana na makosa ya usalama barabarani.

Taarifa zinazosambaa kwa watu mbalimbali na katika mitandao ya kijamii, zinadai kuwa trafiki kwa kila kosa analokamata na kutoza faini katika kila sh 30,000, analipwa Sh 5,000 kama bonasi.

Ufafanuzi juu ya suala hilo ulitolewa Jumatano hii na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga wakati akizungumza na Habarileo ofisini kwake. Alisema hakuna ukweli kwamba askari hao wanapata asilimia fulani kutokana na makosa wanayokamata, bali wamepewa maelekezo ya kukamata makosa mengi kadri wanavyoweza.

“Nafikiri hii inatokana na kukamata makosa mengi, lakini niseme hakuna askari anayelipwa bonasi, wanachokifanya ni kukamata kulingana na makosa tu,” alisema Kamanda Mpinga.

Aidha, alisema zipo taarifa kuwa askari hao wamepangiwa idadi ya makosa, jambo alisema si kweli ila wamepewa maelekezo ya kukamata makosa mengi kadri inavyowezekana, ikiwa ni kwa lengo la kudhibiti ajali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad