Serikali imeombwa kufanya tathmini ya haraka kubaini upungufu wa chakula nchini uliosababishwa na ukame wa muda mrefu.
Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo
ametoa ombi hilo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya
Meru, Elias Nassari katika Usharika wa Usa River, Wilaya ya Arumeru.
Amesema Serikali haitakiwi kungoja hadi watu wafe ndiyo waanze kutafuta chakula.
Dk
Shoo ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Baraza la
Maaskofu Katoliki (TEC), Tarcisius Ngalalekumtwa kuwaandikia maaskofu
wote wa kanisa hilo kuwataka waumini wao wafanye maombi, hija, mfungo
kwa lengo la kukabiliana na ukame unaolikabili taifa.
Vilevile,
hivi karibuni Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) lilitoa wito kama
huo kwa waumini wake, huku Serikali ikisisitiza kuwa hakuna njaa nchini
na kuwa haitatoa chakula cha msaada.