KKKT Nao Watoa Tamko Juu ya Hali ya Njaa Nchini,Waitaka Serikali Ifanye haya..!!!


Serikali imeombwa kufanya tathmini ya haraka kubaini upungufu wa chakula nchini uliosababishwa na ukame wa muda mrefu.


Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo ametoa ombi hilo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Meru, Elias Nassari katika Usharika wa Usa River, Wilaya ya Arumeru.

Amesema Serikali haitakiwi kungoja hadi watu wafe ndiyo waanze kutafuta chakula.

Dk Shoo ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Tarcisius Ngalalekumtwa kuwaandikia maaskofu wote wa kanisa hilo kuwataka waumini wao wafanye maombi, hija, mfungo kwa lengo la kukabiliana na ukame unaolikabili taifa.

Vilevile, hivi karibuni Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) lilitoa wito kama huo kwa waumini wake, huku Serikali ikisisitiza kuwa hakuna njaa nchini na kuwa haitatoa chakula cha msaada.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad