Yanga wanategemea sana mipira ya pembeni, sasa tulijaribu kuangalia watu wanaowachezesha wale watu wa pembeni, tukawakamata na ukiwakamata Yanga kwenye midfield basi unakuwa umeua plan zao wakaishiwa maarifa wakawa hawajui nini cha kufanya sisi tukawa tunatengeneza nafasi na kuzitumia,” anasema kocha wa muda wa Azam Idd Cheche baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi wa kihistoria dhidi ya Yanga.
Kwenye michezo miwili iliyopita Azam haikuonesha kiwango kizuri kiuchezaji huku washambuliaji wake wakishindwa kutumia vizuri nafasi, Cheche amesema tatizo lilikuwa ni umaliziaji na walilifanyia marekebisho ndio maana safu ya ushambuliaji ilikuwa hatari dhidi ya Yanga.
“Tumerekebisha safu ya shambuliaji ndio ilikuwa inasumbua kidogo, tulikuwa tunapata nafasi lakini tuikuwa tunashindwa kuzitumia, movements zilikuwa ndogo kwa hiyo tumelifanyia kazi hili suala la finishing ndio limeleta haya matunda yaliyotokea.”
Azam imefuzu hatua ya nusu fainali na inatarajia kukutana na timu itakayomaliza nafasi ya pili kutoka Kundi A lenye timu za Simba, Taifa Jang’ombe, Jang’ombe Boys na URA ambazo zote zina nafasi.
Hii ndio kauli ya Cheche kuelekea mechi ya nusu fainali: “Yoyote atakaekuja kwenye nusu fainali atakuwa ni mzuri na sisi tumejiandaa kupambana nae tuhakikishe tunavuka tunaingia fainali na kuchukua kombe.”