Korti yaamuru Washtakiwa wa Mauaji ya dada wa Bilionea Msuya Wakatibiwe

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru washtakiwa wa kesi ya mauaji ya Aneth Msuya, wakatibiwe baada ya kukubaliana na madai yao kuwa walipigwa wakiwa mahabusu katika kituo cha Polisi.

Miriam  ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni mjane  wa bilionea Msuya,  aliyekuwa mfanyabiashara wa madini ya tanzanite. Bilionea Msuya pia aliuawa kwa kupigwa risasi Agosti, 2015 eneo la Mijohoroni, kando mwa Barabara ya Arusha–Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Uamuzi wa Mahakama kwa washtakiwa  kwenda kutibiwa unatokana na malalamiko yao waliyoyatoa kupitia kwa wakili Peter Kibatala kuwa walipokuwa mahabusu, waliteswa kwa kupigwa na kulazimishwa kukubali kutenda kosa hilo katika maelezo yao.

Mbali na madai ya washtakiwa hao kuteswa na kuomba Mahakama ifanye uchunguzi na iagize watibiwe, pia Wakili Kibatala alidai hati ya madai ina kasoro za kisheria.

Mahakama ya Kisutu katika uamuzi wake uliotolewa na Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa ilikubaliana na madai ya washtakiwa hao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad