Rais mpya wa Marekani,
Donald Trump aanza kazi hiyo kwa kutia saini amri inayolenga kufanyia
mabadiliko ya mfumo wa afya ulioasiliwa na mtangaulizi wake, Barack
Obama.
Hatua
hiyo inataka wakala mbalimbali kupunguza mzigo wa kiuchumi wa sheria
unaotokana na mfumo wa afya unaojulikana kama Obamacare.
Katika
hotuba yake ya uzinduzi Ijumaa mara baada ya kuapishwa kuwa Rais
aliahidi kutoa kipaumbele katika utendaji wake ‘’kwa kuitanguliza
Amerika kwanza’’ na kumaliza kile alichokiita ‘’ Mauaji ya Amerika’’ ya
kutelekeza viwanda na uwepo uhalifu mkubwa.
Baadaye watu wapatao 200,000 walitarajiwa kujiunga katika maandamano ya wanawake jijini Washington.
Waandaaji
wa maandamano hayo wanasema wanataka kutoa msisitizo juu ya uwepo wa
ubaguzi wa rangi na kukosekana kwa usawa wa kijinsia na mambo mengine
ambayo yanayoonekana kuwa hatarini kukiukwa na utawala wa Trump.
Maandamano
kama hayo tayari yanafanyika Australia na New Zealand na maeneo mengine
mengi yanayoandaliwa katika nchi mbalimbali duniani.
Mwandishi
wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Washington, Barbara
Plett-Usher anasema Rais Trump ameapa kufanya kinachowezekana mara moja
kwa kutumia madaraka aliyonayo kusukuma uhai viwanda kabla ya kurejea
kuandaa muswada wa kupeleka bungeni.
Timu
yake kwa haraka ilibadilisha mfumo wa wavuti wa Ikulu ya Marekani,
White House,ukihusisha nia yake kuzuia mkakati wa Obama kuhusu
mabadiliko ya tabia nchi. Muda mfupi baada ya kushika madaraka kama rais
wa 45 wa Marekani, Trump asiwasilisha mapendekezo ya baraza lake la
mawaziri kwenye Seneti.
Ni kawaida kwavile Dems na Rep wana policy tofauti. Hata Obama alipoingia madarakani alibadilisha aliyoyaweka Bush.Nadhani muendelee kutoa habari za TZ zinazoweza kufichua mabaya na kuikosoa serekali.
ReplyDelete"Kudadeki"nini cha ajabu hapo sasa?
ReplyDelete