KUTENGULIWA Mramba Sio Dawa' Habibu Mchange


Nafikiri kama taifa tumekwama.
Wanasiasa wetu hasa viongozi wa serikali hawaheshimu wataalam wala utaalam na wataalam wetu pamoja na wasomi wanaanza kuingia hofu na kutaka kuwafurahisha Wanasiasa.

Kwa mtazamo wangu, kumuondoa Mramba Tanesco sio suluhisho la tatizo la uendeshaji wa Tanesco.

Tanesco wanasema Gharama za uendeshaji wa shirika Hilo ni kubwa na linaizidi uwezo management.

Tanesco wanasema na ripoti kadhaa zinaonyesha kuwa Wana madeni makubwa.

Na bahati mbaya madeni hayo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.

Ipo haja mahsusi ya serikali kuainisha chanzo kikuu cha kukua Kwa Gharama za uendeshaji Tanesco.

Ipo haja pia ya serikali kuangalia ukubwa huu wa madeni wanayodaiwa Tanesco na vyanzo vyake.

Hii kufurahia Fulani katumbuliwa bado haitoi jibu sahihi la Sababu za Tanesco kutaka kupandisha bei ya umeme.

Kama serikali isipochukua hatua mahsusi na madhubuti lazima bei ipande tu, kama sio Leo kesho na kama sio kesho kesho kutwa, itapanda tu.

Itapanda Kwa Sababu Tanesco wanahisi hiyo inaweza kuwa sehemu ya wao kuwasaidia kupunguza deni na kugharamia uendeshaji wao.

Ushauri wangu ni Serikali kupitia upya mikataba yote inayoipa mzigo wa madeni Tanesco.

Waipitie na watujulishe Watanzania kupitia wawakilishi wetu au moja Kwa moja kila aina ya mkataba na changamoto zake.

Kisha kama taifa tupige mstari na kuweka way foward ya pamoja.

Kinyume na hapo Leo Mramba katenguliwa, na kesho mwengine atatenguliwa na kutenguliwa na kutenguliwa.

Lakini je kutenguliwa huku kunajibu Sababu za wao kupandisha bei? ...

Kuna haja Sasa ya sisi kama Taifa kutibu chanzo cha tatizo sio kuhangaika na matokeo ya tatizo.

Habibu Mchange
Mwananchi.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Habibu Mchange nafikiria msimamo wako sio wenye masilahi na walalahoi ambacho ndicho mkuu wa nchi anakisimamia lazima huyo bosi wako unayemtetea angesoma nyakati sio madeni na hasara ya Tanesco iwegharimu watanzania wenye maisha ya chini kama angelikuwa na nia nzuri huyo bosi angefata taratibu halafu ingetolewa uamuzi na raisi kupandisha au kushusha bei na yeye angekuwa safe side enzi ya kambare kila mmoja ana sharubu umepita na ndio waliotufikisha hapa sasa nchi imepata mtu wakuisimamia nchi hii ya watu masikini

    ReplyDelete
  2. mzee magu yupo sahihi kabisa hata kama shirika lina deni kubwa kwaiyo solution ni kuwaumiza wanachi tu ili walipe deni hilo?na inakuaje shirika linazidi kuwa na deni kubwa wakat hatutumii umeme bure kuna haya ya kutumbua watu wasomi wapo wengi sana na mbinu mbalimbali za kutatua matatizo zipo mi siamini kama mikataba ndio inafanya deni liendelee kuwa kubwa.toa kitu weka kitu mjomba endelea kuwatumbua kwa raha zako watu wanafanya kazi kwa mazoea sana

    ReplyDelete
  3. Sawa sawa kutenguliwa ndio mtatia akili sasa, kuchukua tu maamuzi hata bila kuishirikisha serikali, alafu mnataka wananchi walalahoi wangaike zaidi, na kuilaumu serikali, na mnajua kabisa Tanesco ni Mali ya umma, nyie mfaidike, mzibe mapengo yenu mnayowaibia wananchi, alafu wananchi wangaike, Serikali ya sasa haitaki mchezo, ni khaki bin khaki

    ReplyDelete
  4. Nadhani anachotaka Muheshimiwa Rais ni kwamba anataka mtu atakayekuja na road-map, ili shirika liweze kujiendesha kwa faida, kuongeza bei bado si suluhisho, lazima uangalie kama makosa yalifanyika wapi na wafanyaje kuyarekebisha bila kumuathiri
    mwananchi wa kawaida, huwezi kuwa na plan ya kujenga uchumi wa viwanda kama huduma muhimu kama umeme, mafuta zipo juu. kama madeni naungana na wenzangu wanaouliza yametoka wapi?? so later wakitengeneza madeni mengine huko watakuja kuongeza bili?

    ReplyDelete
  5. Kama ni kweli hilo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lina ukwasi wa kiasi cha kushindwa kuendesha shughuli zake mbalimbali za usambazaji umeme na projects nyinginezo, je ni kwa nini walipane zile posho za kiinua mgongo yani bonus kiasi cha shilingi milioni 40 mpaka milioni 50 kila mwaka?????........ni kwa nini hizo pesa zisipelekwe kwenye maeneo endelevu ya kuwapatia wananchi umeme wa uhakika ikiwamo kusambaza umeme huko vijijinii????

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad