Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewasihi viongozi wa vyama vya
wapinzani kujikita katika siasa safi na uongozi bora, kwa kuachana na
matamko ya uongo yanayosababisha taharuki katika nchi na kuchonganisha
wananchi na serikali yao, kwa kuwa vitendo hivyo havina manufaa kwa
mustakabali wa maendeleo ya taifa.
Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Huphrey
Polepole, wakati akizungumza na waandishi wa habari, leo Januari 17,
2017, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es
Salaam, kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Kichama.
Polepole amsema, wapinzania wamekuwa wakitumia matatizo ya
wananchi na kutoa matamko ya uongo ili kutia nchi katika taharuki kwa
lengo la kujitafufia umaarufu wa siasa vitendo ambavyo alisema,
havisaidii wananchi wala wanasiasa wa vyama hivyo katika kuleta
maendeleo ya nchi.
Alisema, mbali na matamko ya viongozi wa vyama hivyo
kutosaidia, katika ujenzi wa maendeleo yamaendeleo ya nchijambo ambalo
alisema za kueneza maneno ya yasiyofanyiwa utafiti kwa lengo la
kusababisha taharuki kwa wananchi, jambo ambalo alisema, si miongoni mwa
siasa safi wala uongozi bora.
Polepole alisema, wapinzani wamekuwa wakifanya siasa za
aina hiyo wakiwa wanajua ubaya wake, kwa kuwa wao lengo lao ni kujaribu
kuchonganisha wananchi na serikali hata pale ambapo serikali inaonyesha
juhudi za dhali za kuijenga Nchi yenye uchumi imara wa viwanda.
“Nawaonba Watanzania tuwapuuze wanasiasa wa vyama hivi,
tuendelee kuiunga mkono serikali, ili itimize mipango na malengo
iliyoweka, ikiwemo kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi kwa kuwa nchi
ya viwanda, hali ambayo itasaidia sana kutukwamua Watanzania kutoka
katika umasikini”, alisema Polepole.
Polepole alitaja kuwa miongozi mwa mambo ambayo katika
kipindi hiki wanayatumia kupotosha ili kujaribu kuletea taharuki
wananchi ni pamoja na kueneza propaganda kuwa Tanzania imekumbwa na baa
la njaa na pia kutumia matatizo waliyopata wananchi wakati wa janga la
tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera kama mtaji wao
kisiasa.
“Kwanza mjue, kutungaza taarifa ambazo zitaleta taharuki
katika jamii ni kosa la jinai, lakini pia inajulikana na wenyewe
wanajua, kwamba Duniani kote zipo taratibu ya utangazaji wa majanga
katika nchi yoyote. Baa la njaa ni janga kubwa linapofikia kiwango
kibaya, mwenye mamlaka ya kutangaza ni Mkuu wa nchi”, alisema Polepole
na kuongeza;
Alisema, Tanzania haijawahi kupata njaa yenye kiwango cha
kuitwa baa la njaa, katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, hivyo
wanaojaribu kutangaza kuwa Nchi ipo katika baa la njaa ni kushindwa
kufanya siasa safi na kukosa uongozi bora kama ilivyo CCM ambayo mambo
hayo inayo.
“Ingawa tumekuwa na tatizo la njaa katika sehemu chache za
na kuwepo upungufu wa mvua katika maeneo kadhaa ya nchi hali ambayo
inaweza kusababisha upungufu wa chakula katika maeneo husika, bado hili
siyo baa la njaa. Na kwa kuwa hili serikali inalijua inaendelea kuweka
mazingira mazuri ili kuweza kupelekwa vyakula maeneo yote kuondoa uhaba,
na kipindi hiki hatujafikia huko”, alisema Polepole.
“Baada ya kuona hali ipo hivi nilitarajia viongozi wote
bila kujali vyama , tuhimize wananchi kutumia chakula vizuri wasikitumie
katika mambo ya anasa au kukiuza hovyo, lakini wao wanakimbilia
kutangaza baa la njaa wakati njaa yenyewe haijatokea, hawa watu wa ajabu
sana’, alisema Polepole.
Alisema, kila kiongozi anayeongozwa na misingi ya uongozi
bora na mzalendo kwa nchi yake, analo jukumu la kuwahamasisha wananchi
kutunza vyakula walivyonavyo.
Kuhusu tetemeko lilitokea Bukoba na kusababisha uharibifu
na vyumba za watu na miundombinu mbalimbali alisema kama ilivyo
ulimwenguni kote, inapotokea mambo haya ya majanga serikali hujenga
uwezo wake kwanza ili kusaidia wananchi wake.
“Baada ya tetemeko lile, Serikali ilichofanya ni kujengea
uwezo wa wananchi wasiwe mbali na huduma ndiyo maana ikaimarisha
miundombinu ya elimu, afya na barabara, kwa sababu watu waendelee kupata
huduma”. alimalizia Polepole